Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-21 16:01:38    
Bibi Gu Xiulian azungumzia uhusiano kati ya michezo ya Olilmpiki na wanawake

cri

Shughuli za wiki ya utamaduni wa wanawake wa China na Uingereza zilianza tarehe 10 mwezi Februari mwaka 2008. Ujumbe unaoongozwa na naibu spika wa bunge la umma la China ambaye pia ni mwenyekiti wa shirikisho kuu la wanawake wa China Bibi Gu Xiulian, uliwasili London Uingereza na kushiriki shughuli hizo.

Baada ya kuwasili London, Bibi Gu Xiulian alihojiwa na waandishi wa habari wa shirika la habari la China Xinhua. Alisema, michezo ya Olimpiki yenye historia ya zaidi ya miaka 100 inaleta fursa nyingi kwa wanawake, kuwahamasisha, na kuwashirikisha vizuri wanawake siyo tu kutasaidia kutimiza ndoto ya michezo ya Olimpiki, bali pia kutahimiza zaidi maendeleo ya wanawake.

Katika mwezi Agosti mwaka huu michezo ya 29 ya Olimpiki itafanyika mjini Beijing, na mwaka 2009 London pia itakuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki. Michezo ya Olimpiki ni kama daraja jipya kati ya wanawake wa China na Uingereza. Michezo ya Olimpiki ni jambo muhimu linalofuatiliwa na wanawake wa China na Uingereza, hivyo kauli mbiu muhimu ya wiki hiyo ya utamaduni wa wanawake wa China na Uingereza ni "wanawake na michezo ya Olimpiki"

Bibi Gu Xiulian anaona kuwa wanawake wa China wanafanya juhudi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii ya China, na pia wamenufaika maendeleo hayo. Wachezaji wa kike wa China walipata nafasi ya kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki baada ya kupita muda mrefu na kupata matatizo mengi. Mwaka 1936, kwa mara ya kwanza China ilituma wachezaji wa kike kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki. Baada ya China mpya kuzaliwa, shughuli za michezo nchini China na shughuli za wanawake kushiriki kwenye michezo zilipata maendeleo makubwa.

Tangu Beijing ilipopata nafasi ya kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki, wanawake wa China walishiriki katika kazi mbalimbali za maandalizi ya michezo ya Olimpiki. Wanawake wanaoshughulikia mawasiliano ya umma, utalii, afya, elimu, mambo ya viwanda na biashara, mambo ya ushuru na mambo ya fedha walifanya juhudi kuinua uwezo wao wa kazi, ili kuweka msingithabiti wa kutoa huduma kwenye michezo ya Olimpiki.

Bibi Gu Xiulian pia aliongeza kuwa, michezo ya Olimpiki itakuwa ni jukwaa la mawasiliano ya harakati za wanawake na shughuli za wanawake na fursa ya kuhimiza ushirikiano kati ya wanawake wa nchi mbalimbali. Katika michezo ya Olimpiki ya Beijing, dunia nzima itaona historia ndefu na utamaduni mbalimbali wa China, na mafanikio waliyopata wananchi wa China tangu China ilipoanza kufungua mlango, na pia itaona mafanikio makubwa waliyopata wanawake wa China katika kujipatia haki, uhuru na maendeleo.

Bibi Gu Xiulian pia alisema kuwahimiza wanawake watimize ndoto ya michezo ya Olimpiki, na kufanya michezo ya Olimpiki ihimize maendeleo ya wanawake, ni mambo muhimu ya shirikisho la wanawake wa China kuhimiza wanawake washiriki kwenye michezo ya Olimpiki.

Bibi Gu Xiulian pia alisisitiza kuwa, serikali ya China inatilia maanani maendeleo ya wanawake, na kuuchukua usawa wa kijinsia kuwa sera ya kimsingi ya kuhimiza maendeleo ya jamii. Kulinganishwa na hali ya miaka 10 iliyopita, usawa wa kijinsia nchini China umepata maendeleo makubwa, sheria na kanuni za kulinda maslahi ya wanawake zinaboreshwa,

Balozi wa China nchini Uingereza Bibi Fu Ying anaona kuwa, shughuli za wiki ya utamaduni zikiwemo mkutano wa Baraza la wanawake na michezo ya Olimpiki, mkutano wa mawasiliano kati ya wanaviwanda wanawake wa China na Uingereza, maonesho ya picha za wanawake wa China zote zinaonesha sura ya kujiamini na kujiendeleza za wanawake wa China.

Shughuli za wiki ya utamadumi wa wanawake wa China na Uingereza ulifanyika kuanzia tarehe 10 hadi tarehe 17 mwezi Februari. Shughuli hizo zilikumbusha historia na maendeleo ya uhusiano kati ya wanawake wa China na Uingereza na michezo ya Olimpiki ya zana za hivi sasa, kujadili mambo halisi ya moyo wa Olimpiki na kuzungumzia mustakabali wa maendeleo ya wanawake kutokana na kuhamasishwa na moyo wa Olimpiki. Lengo kubwa la shughuli hizo ni kuimarisha mawasiliano kati ya wanawake wa China na Uingereza na maelewano kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Idhaa ya kiswahili 2008-02-21