Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-02-25 15:46:06    
Yuantouzhu, lulu iliyoko kwenye ziwa Taihu

cri

Ziwa Taihu, ambalo liko katika mji wa Wuxi, mkoani Jiangsu, sehemu ya mashariki ya China, ni moja kati ya maziwa matano makubwa ya maji baridi ya nchini China. Kwenye kando la kaskazini magharibi ya ziwa Taihu, kuna sehemu moja ya ardhi iliyojitokeza kwenye ziwa hilo, kwenye sehemu hiyo ya ardhi kuna jiwe moja kubwa mfano wa kobe mkubwa anayeinua kichwa juu, hivyo sehemu hiyo inaitwa kuwa Yuantouzhu, maana yake ni ardhi yenye kichwa cha mungu wa kobe.

Sauti unayosikia sasa ni ya wimbo maarufu ulioenea sana huko toka miaka 50 iliyopita unaoitwa "Mashua ya Ziwa Taihu". Wimbo huo unasimulia mandhari nzuri ya Yuantouzhu. Watu wa ujumbe wa wakazi wa sehemu ya "bwawa la jua na mwezi" ya mkoa wa Taiwan ulipoitembelea sehemu ya Yuantouzhu, waliimba wimbo huo kwenye kando ya ziwa la Tai. Kiongozi wa ujumbe huo, Bw. Chen Zhensheng alisema, wimbo la "Mashua ya Ziwa la Tai" unawafanya wakazi wa mkoa wa Taiwan walipende ziwa Taihu.

"Wimbo huo uliletwa kisiwani Taiwan zaidi ya nusu karne iliyopita, na ulienezwa na wakazi wa huko. Leo tumefika kwenye sehemu ya Yuantouzhu ya ziwa Taihu, ambalo tunalipenda mioyoni mwetu, tumeshuhudia mandhari nzuri ya ziwa Taihu."

Mwaka 1918, bustani zilianza kujengwa kwenye sehemu ya Yuantouzhu, ambapo watu maarufu, maofisa wakubwa na makabaila wengi walikwenda huko kujenga nyumba binafsi zenye bustani. Baada ya ujenzi uliofanywa huko kwa muda wa miaka kumi kadhaa, hivi sasa sehemu yenye mandhari nzuri ya Yuantouzhu imefikia hekta 300 hivi, na kuwa moja ya bustani kubwa zenye vilima na vijito za kusini mwa mto Changjiang.

Yuantouzhu ni mahali pazuri kabisa pa kuangalia vivutio vya milima na ziwa Taihu katika eneo lile. Jiwe lile kubwa linalojitokeza kwenye ziwa Taihu, ambalo pande zake tatu zinazungukwa na maji, watalii wakikaa kwenye jiwe la Yuantouzhu, wanaweza kuona mashua nyingi zenye matanga meupe zilizoko mbali, na jinsi ilivyo ni kama michoro ya mandhari. Kila mwaka kuna watalii zaidi ya milioni 3 wa nchini China na wa nchi za nje, wanaoitembelea sehemu ya Yuantouzhu, ambao wengi wao wanavutiwa na mandhari nzuri ya sehemu hiyo, mtalii kutoka mkoa wa Taiwan, Bw. Zhong Rongji, alisema,

"Msomi wa fasihi, Bw. Guo Moruo aliandika hati ya maneno ikisema, 'sehemu inayopendeza zaidi kwenye ziwa Taihu, siyo mahali pengine ila tu ni sehemu ya Yuantouzhu', kiongozi wa jumuiya ya dini ya kibudha ya China, Bw. Zhao Puchu alisema, baada ya kuitembelea sehemu ya Yuantouzhu kuwa, sehemu hiyo ni mahali penye mandhari nzuri kuliko peponi, maneno yake yamedhihirisha uzuri wa ziwa Taihu na uzuri wa Yuantouzhu. Nimefika hapa hivi karibuni, na nitatumia muda mwingi katika matembezi yangu kwenye ziwa Taihu ili kutimiza matarajio yangu ya miaka mingi."

Kama alivyosema Bw. Zhong Rongji, mandhari nzuri zinasifiwa katika mashairi na kuchorwa kwenye michoro. Baada ya kufanya juhudi kwa miaka mingi, hivi sasa hati za maneno na michoro husika ya mandhari iliyokusanywa na sehemu ya mandhari ya Yuantouzhu imekuwa mingi, idadi yake na sifa zake vinalingana na kiwango cha jumba dogo la makumbusho, na vitu vingi hivyo vya kiutamaduni viliandikwa au kuchorwa na mabingwa maarufu. Sehemu ya Yuantouzhu inafanya shughuli za sanaa kila mwaka, ambapo watalii licha ya kuweza kuburudishwa na mandhari nzuri ya ziwa Taihu, wanaweza kushuhudia utamaduni mkubwa wa huko.

Mbali na hayo, sehemu ya Yuantouzhu imehifadhi merikebu za kale zenye milingoti 7 ya enzi ya Song ya miaka zaidi ya 1,500 iliyopita. Merikebu hiyo ina urefu wa mita 25 na upana wa zaidi ya mita 5, na urefu wa mlingoti mrefu zaidi wa merikebu hiyo ni mita 17, merikebu hiyo ilitengenezwa kwa miti ya mivinje, na ina umbo la kupendeza. Katika miaka ya hivi karibuni, sehemu hiyo ya mandhari iliunda mashua mpya kwa kuiga mfano wa merikebu hiyo ya kale, na watalii wanaweza kupanda kwenye mashua hizo na kuangalia vivutio vya sehemu hiyo. Kila mashua ina viti vya mbao zaidi ya 30, ndani na nje ya mashua hizo zinapambwa kama mashua halisi za wavuvi, licha ya kuangalia mandhari ya ziwa Taihu, watalii wanaweza kupandisha matanga ya mashua, kushika usukani na kuvua samaki wakielekezwa na wavuvi, tena wanaweza kula mazao ya majini ya ziwa Taihu yakiwemo samaki weupe, kamba weupe na aina ya samaki ya dagaa. Dada Fan Li, ambaye hivi sasa anasoma mjini Wuxi, alisema,

"Safari hii, nimepanda kwenye mashua yenye milingoti 7, nimevutiwa sana na mandhari nzuri ya ziwa Taihu, wazee walisema, miaka mingi hawajaona mazingira hayo. Ziwa Taihu ni zuri sana kama linavyoonekana kwenye michoro, nimevutiwa sana na mazingira hayo, ninaona hapa ni mahali pa kustahili kutembelewa."

Sehemu ya Yuantouzhu ina uzuri wa aina mbili kwa pamoja, uzuri wa sanifu na uzuri wa ukubwa wa mandhari ya ziwa. Huko kuna kundi kubwa la milima na maji ya ziwa yanayoweza kuonekana kwa upana mkubwa, pamoja na matanga ya mashua zilizoko mbali yanayoonekana kuwa madogo, kama inavyoonekana kwenye michoro ya sanaa; pia kuna madaraja madogo na mifereji yenye maji yanayotiririka, miti, nyumba, vijito na mashamba; kuna mandhari nzuri ya bustani za sehemu ya kusini ya China; pia kuna huduma na zana kamili za burudani zikiwemo za chakula, nyumba za wageni, ununuzi wa vitu vya mahitaji na mawasiliano, licha ya hayo kuna utamaduni mkubwa kuhusu matembezi ya watu mashuhuri wa enzi mbalimbali, maneno yaliyochongwa kwenye mawe, hati za maneno, michoro na hadithi. Endapo utapata nafasi ya kuja China, usisahau kuitembelea sehemu hiyo.

Idhaa ya kiswahili 2008-02-25