Tarehe 7 mwezi Februali ilikuwa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China katika kalenda ya kilimo ya China, ambayo ni sikukuu kubwa kabisa ya jadi ya wachina. Wakati wa sikukuu hiyo wachina wanapenda kutembelea magulio ya mahekalu. Magulio hayo yanayofanyika katika sikukuu karibu na mahekalu yanaunganisha shughuli za burudani, utalii na mauzo ya bidhaa, na pia ni mahali muhimu pa kuonesha utamaduni wa jadi wa China. Beijing ikiwa ni mji mkuu wa utamaduni wa China, magulio yake yanayofanyika karibu na mahekalu yanajulikana zaidi hapa nchini.
Magulio ya mahekalu ya Beijing ni kama vichochoro na nyumba za jadi za Beijing ambazo ni alama ya historia ya mji huo. Magulio ya mahekalu ya Beijing yalianza katika enzi ya Liao ya kabla ya zaidi ya miaka elfu moja iliyopita, mwanzoni kabisa yalikuwa shughuli za kidini za kufanya matambiko zenye shughuli kidogo za mauzo ya bidhaa. Lakini katika siku ya leo, magulio ya mahekalu yameendelezwa kuwa mahali pa kusanyika pamoja na kununua bidhaa katika siku za sikukuu.
Gulio la hekalu la Ditan ni moja ya magulio maarufu ya mjini Beijing lenye shughuli nyingi za burudani za jadi zilizopendwa sana na watu zilifanyika. Hekalu la Ditan, ambalo eneo lake ni hekta zaidi ya 40, lilijengwa katika mwaka 1530, lilikuwa mahali pa kufanya sherehe ya kumtambika mungu wa ardhi kwa wafalme wa kale. Bw. Zhang Jinsong, ambaye ni ofisa wa kamati ya maandalizi ya shughuli za gulio la hekalu la Ditan, alisema, katika miaka ya karibuni, idadi ya watu waliotembelea gulio la Ditan ilifikia kiasi cha milioni moja kila mwaka, watalii waliotoka mikoani hata kutoka nchi za nje, wanavutiwa na hali maalumu ya gulio la Ditan. Alisema,
"Gulio la hekalu la Ditan ni kama dirisha linaloonesha jadi ya kisasa ya wachina, halaiki ya watu wanapita kwenye majumba ya hekalu yenye kuta za rangi nyekundu, kuezekwa kwa vigae vya rangi ya kijani na yenye misonobali na mivinje mingi pembezoni mwake, watu wanavutiwa na aina mbalimbali za chakula na bidhaa za jadi pamoja na shughuli za kiutamaduni. Watalii wanaweza kuona mambo mengi ya jadi ya wakazi kwenye hekalu la kifalme, hususan wageni wa nchi za nje wanaweza kuona mazingira ya utamaduni wa jadi ya China."
Shughuli za gulio la hekalu la Ditan la mwaka huu zilifanyika toka tarehe 6 hadi tarehe 13 mwezi Februali. Mwaka huu, gulio la hekalu la Ditan limeonesha umaalumu wa mitaa ya wakazi wa Beijing, ambao kuta na vigae ni za rangi ya kijivu, na kufanya watalii wajione wako kwenye mitaa ya wakazi wenyeji wa Beijing. Katika siku za kufanyika shughuli za gulio, kila siku asubuhi hufanya maonesho ya tambiko la mungu wa ardhi, ambapo watu wanaweza kuona mambo yote yaliyofanywa na wafalme wa enzi ya Qing ya zaidi ya miaka 100 iliyopita, ya kuomba mundu wa ardhi kubariki watu wawe na usalama, hali nzuri ya hewa na mavuno mazuri. Licha ya hayo, watalii wanaweza kushuhudia jadi na mila ya wakazi wenyeji wa Beijing. Maonesho ya mila na jadi ya wakazi wenyeji wa Beijing yaliyofanyika kwenye gulio la hakelu la Ditan, yalionesha vitu zaidi ya elfu moja vinavyotumiwa na wenyeji wa Beijing, na kila moja ya vitu hivyo ni kama ufunguo wa kufungua kumbukumbu za wenyeji wa Beijing. Mbali na hayo, gulio la Ditan lilifungua kiwanja cha maonesho ya utamaduni usio wa vitu, ambapo aina 18 za ufundi wa jadi zilizoorodheshwa kwenye orodha ya utamaduni usio wa vitu, zilioneshwa kwenye kiwanja cha maonesho.
Mwaka huu ni mwaka wa panya katika kalenda ya kichina, gulio la Ditan lilitengeneza kitu cha baraka chenye umaalumu wa mwaka wa panya, ambacho ni kinyago cha panya kilichotengenezwa kwa udongo wa ufinyanzi na kwa ufundi wa jadi, na baadhi ya vinyago vya panya viliuzwa kwenye gulio. Panya wawili wenye maumbo ya kupendeza wakiwa wanasimama wima, ambao mmoja ni wa rangi nyekundu na mwingine ni wa rangi ya manjano, wanaweka miguu ya mbele nyuma ya miili yao na kunyanyua vichwa. Katika siku za kufanyika kwa gulio la Dita, panya hao wawili wakubwa wakisimama kwenye hekalu la Ditan na kuwalaki wageni waliotoka sehemu mbalimbali. Ili kuunganisha shughuli za ghulio la hekalu na michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008, ghulio hilo lilionesha mambo mengi ya michezo ya Olimpiki. Ofisa wa kamati ya maandalizi ya shughuli za gulio la hekalu la Ditan, Bw. Zhang Jinsong alisema,
"Mwaka 2008 ni mwaka wa michezo ya Olimpiki, wilaya ya mashariki ya Beijing ni wilaya pekee kati ya wilaya nne zilizoko kwenye sehemu ya katikati ya mji wa Beijing inayofanyika michezo ya ndondi ya Olimpiki, ili kuwawezesha watu kuona hali ya michezo ya ndondi, gulio la Ditan lilijenga jukwaa la mabondia, ambalo watu wanaotembelea gulio la Ditan wanaweza kufanya mazoezi na kupata mafunzo ya mabondia maalumu, au kupimana nao."
Katika mji wa Beijing, kuna magulio ya mahekalu kumi kadhaa wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, na kila gulio lina shughuli nyingi na umaalumu wake, katika magulio hayo, licha ya kuweza kushuhudia mila na desturi ya wakazi wa Beijing, bali pia unaweza kufurahishwa na hali ya shamrashamra ya sikukuu. Kwenye bustani ya sanamu za kimataifa ya Beijing iliyoko sehemu ya magharibi ya Beijing, mwaka huu lilifanyika gulio lenye shughuli za kiutamaduni za mwaka wa China. Kiongozi wa kamati ya maandalizi ya gulio la utamaduni wa mwaka mpya wa jadi wa China, Bw. Du Long alisema, magulio ya mahekalu yameonesha bidhaa na utamaduni maalumu wa mikoa na miji sita mikubwa ya sehemu za mashariki, magharibi na kati za China.
"Kauli-mbiu ya gulio letu la hapa ni utamaduni wa mwaka mpya wa jadi wa China, inaonesha shughuli mbalimbali za sehemu na makabila mengi ya China katika kipindi cha sikukuu ya Spring. Hivi sasa tumepaga maonesho murua katika bustani nyingi za Beijing, ambayo yanashirikiwa na mikoa tano ya Shanxi, Hubei, Yunnan, Guizhou na Guangdong. Mikoa hiyo mitano inawakilisha umaalumu wa mila na jadi ya sehemu za mashariki, kusini, magharibi, kaskazini na kati za China, licha ya hayo, watu wanaweza kuona na kuonja chakula, bidhaa na ufundi wa maduka kumi kadhaa maarufu ya miaka mingi na wa mabingwa wasanii."
Pamoja na kuinuka kwa utandawazi wa kimataifa, magulio ya Beijing licha ya kudumisha utamaduni na jadi za China, pia yamekuwa na mambo mengi ya kimataifa. Kwenye bustani yenye shughuli nyingi za burudani ya Shijingshan iliyoko sehemu ya magharibi ya Beijing, kila mwaka inaandaa "gulio la kimagharibi", ambalo watu wanaweza kuhisi hali na mazingira ya nchi za nje na furaha ya sikukuu ya nchi za magharibi.
Idhaa ya kiswahili 2008-03-03
|