Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-07 16:17:54    
Utamaduni wa makabila mbalimbali ya China waleta mfano wa masikilizano

cri

Balozi wa Eritrea nchini China Bw. Tseggai Tesfatsion alipohojiwa na waandishi wa habari hivi karibuni alisema, anasifu utamaduni wa makabila mbalimbali ya China na maoni ya wananchi wa China kuhusu kujenga jamii yenye masikilizano. Bw. Tesfatsion alisema "napenda kutazama vipindi kuhusu makabila madogomadogo ya China vinavyooneshwa kwenye channel 9 ya kituo cha CCTV, hasa vipindi vinavyoeleza utamaduni wa sikukuu za jadi za makabila mbalimbali ya China." Bw. Tesfatsion alikuja nchini China mwaka 2003 baada ya kuteuliwa kuwa balozi wa Eritrea nchini China. Eritrea iko katika sehemu ya kaskazini mashariki mwa Afrika na ina makabila tisa. Bw. Tesfatision alisema ana matumaini ya kupata maarifa ya kuishi pamoja kwa makabila mbalimbali ya China, na baada ya kurudi nyumbani anaweza kuyatumia maarifa hayo katika mambo ya makabila ya Eritrea.

Bw. Tesfatsion anavutiwa na wazo la masikilizano lililoelezwa kwenye utamaduni wa jadi wa Cofucianism wa China, na alisema Afrika inaweza kuwa sehemu moja wa dunia yenye masikilizano. Alipokumbusha maisha yake ya miaka mitano ya kuwa balozi wa Eritrea nchini China, alisema China inamhemshimu kila ofisa wa kidiplomasia bila ya kujali anatoka nchi iliyoendelea au nchi inayoendelea. Alisema "ingawa nimetoka kwenye nchi ndogo, lakini ninaheshimiwa kama mabalozi wengine."

China na Eritrea zilianzisha uhusiano wa kibalozi tarehe 24 mwezi Mei mwaka 1993. Bw. Tesfatsion alisema uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelezwa vizuri. Pia alisema Eritrea inakaribisha zaidi uwekezaji kutoka China kuliko misaada ya vyakula. "uwekezaji wa muda mrefu utatusaidia kuendeleza uchumi na tunataka kuagiza mashine na teknolojia za sayansi mingi kutoka China."

Hivi sasa Eritrea inapokea watalii 300 kutoka China kila mwaka, ambao wengi ni wafanyabiashara. Bw. Tesfatsion alisema Eritrea sasa inafanya juhudi ili kuweka mazingira ya usalama ya utalii kwa wageni.

Habari nyingine zinasema, balozi wa China nchini Misri Bw. Wu Chunhua hivi karibuni katika tafrija ya kusherehekea mwaka mpya ya waandishi wa habari wa China na Misri, alisema katika mwaka 2007 uhusiano kati ya China na Misri ulipata mafanikio makubwa na mawasiliano na ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali uliendelezwa vizuri. Bw. Wu Chunhua alisema ziara ya spika wa bunge la umma la China Bw. Wu Bangguo nchini Misri na ziara ya spika wa bunge la umma la Misri Bw. Surue nchini China, zimeimarisha msingi wa kisiasa wa pande hizo mbili. Thamani ya biashara kati ya China na Misri imezidi dola za kimarekani bilioni 4.5 ambayo ni ya kiwango cha juu kabisa katika historia.

Bw. Wu Chunhua alisema ubalozi wa China nchini Misri utashirikiana na vyombo vya habari vya Misri na China katika mwaka mpya na kufanya juhudi kuhimiza ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Misri, maendeleo ya uhusiano kati ya China na nchi za kiarabu, na kati ya China na Afrika.

Mwenyekiti wa shirika la urafiki wa Misri na China Bw. Yusuf Wali, katika pongezi zake alisifu sana urafiki wa jadi uliopo kati ya Misri na China. Alisema rais Mubarak wa Misri aliwahi kuzuru China mara tisa na alisisitiza mara nyingi umuhimu wa kuendeleza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya China na Misri. Bw. Wali anapenda uhusiano kati ya nchi hizo mbili hasa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara uimarishwe.

Habari nyingine zinasema balozi wa Shelisheli nchini China Bw. Philippe Le gall, hivi karibuni alipohojiwa na mwandishi wa habari wa China alisema, anaandika kitabu kuhusu China na anaeleza uelewa na upendo wake kwa utamaduni wa jamii wa China tangu ashike madaraka ya ubalozi. Alisema "kitabu hicho kinaeleza maoni yangu kuhusu China." Ingawa kitabu hicho kimeandikwa kwa lugha ya kifaransa, lakini Bw. Le gall alisema atakitafsiri kwa lugha ya kichina ili watu wengi zaidi wa China waweze kukisoma.

Bw. Le gall alikuja hapa China zaidi ya miezi minane iliyopita, aliona jamii ya hivi sasa ya China ina nguvu na wachina wanafanya juhudi za uvumbuzi. Wasanii wa kundi la watangulizi la China kwenye kiwanda cha sanaa cha 798 na wachuuzi wa soko la mabaki ya utamaduni wa Pan Jiayuan wanamshangaza Bw. Le gall. Alisema,

"ninavutiwa na sanaa na utamaduni wa China, ninataka kuishi nchini China mpaka nitakapostaafu."

Kutokana na elimu ya Ulaya, maisha barani Afrika na maarifa barani Asia, Bw. Le gall anaona yeye ni kama chombo cha kuchanganya utamaduni. Alisema "ingawa nimewahi kutembelea nchi nyingi, lakini utamaduni na jamii ya China vinavyobadilika siku hadi siku vinanivutia zaidi." Alisema China inaelekea kuwa ya kisasa zaidi, kasi yake hiyo ni kubwa zaidi kuliko nchi nyingine.

Baada ya kuja China, Bw. Le gall alianza kujifunza lugha ya kichina. Alisema: "lugha ya kichina ni ngumu sana, mpaka sasa siwezi kuitumia, najisikia vibaya sana." Lakini aliendelea kujifunza lugha ya kichina kila siku alipokuwa anaendesha gari. Anafurahi sana kusikiliza vipindi vya muziki wa kisasa wa kichina ingawa haelewi maneno ya wimbo.

Samani za kale za enzi za Ming na Qing za China, vyombo vya kauri, mapambo ya fedha ni vitu anavyopenda Bw. Fe gall. Alipokumbusha kuhamia nchini Shelisheli kutoka Ufaransa, alisema: "nilitaka kutazama bahari na kuondokana na mazingira yenye makelele mijini." Lakini sasa amekuwa na humu tena ya kuishi kwenye mji mkubwa kutokana na maisha ya mjini Beijing.

Bw. Le gall alizaliwa katika familia ya mfanyabiashara wa vito, mkoani Bretani kaskazini mwa Ufaransa, alipenda sanaa na utamaduni wakati alipokuwa mtoto, na aliandika kitabu cha "bustani ya mfalme" kinachoeleza maisha yake nchini Shelisheli kwa miaka 16. Aliwahi kuwa mshauri wa utamaduni na mshauri wa mambo ya kidiplomasia wa serikali ya Shelisheli.

Idhaa ya kiswahili 2008-03-07