Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-03-13 15:42:53    
Mjumbe mwanamke wa Mkutano wa Bunge la Umma kutoka Uwanda wa juu wa Pamirs

cri

Yeye ni mjumbe pekee wa kabila la wakirgiz wa bunge la umma la China. Kutokana na sheria ya uchaguzi wa China, kabila la wakirgiz ambalo idadi ya watu wake ni zaidi ya laki 1.6 hivyo limepata nafasi ya kuchagua mjumbe mmoja. Na Maria Mati alichaguliwa kuwa mjumbe pekee wa kabila hilo.

Baada ya kifungua kinywa, Bibi Maria alifungua kompyuta na kuongeza zaidi maneno ya hotuba yake itakayotolewa siku hiyo asubuhi.

Ingawa Bibi Maria ana umri wa miaka 37, lakini amekuwa mjumbe wa bunge la umma la China mwenye uzoefu. Alichaguliwa kuwa mjumbe wa bunge la awamu ya 10 la umma la China mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 32. Wakati huo, yeye ni kada wa kijiji cha tarafa inayojiendesha ya kabila ya wakirgiz ya Qizilsu la mkoa wa Xinjiang. Mliyomsikia ni hotuba aliyotoa Bibi Maria kwenye majadiliano ya wajumbe wa Xinjiang waliohudhuria mkutano wa bunge la 10 la umma la China miaka miwili iliyopita.

Bibi Maria alikumbusha hali ya miaka miwili iliyopita akisema, tarehe 8 mwezi Machi mwaka 2006 ilikuwa siku ya kimataifa ya wanawake. Siku hiyo bibi Maria alifurahi sana, kwani waziri mkuu Wen Jiabao alikwenda kusikiliza maoni ya wajumbe wa Xinjiang waliohudhuria mkutano wa bunge la umma la China. Baada ya kusikiliza hotuba za wajumbe kadhaa, waziri mkuu Wen Jiabao alipendekeza kumpa mjumbe wa shina fursa ya mwisho ya kutoa hotuba. Alipotazama orodha ya wajumbe aliona jina la bibi huyo, akisema, "hebu, tusikilize bibi Maria aseme." Bibi Maria alipokumbusha alisema,

"Wakati huo nilitoa pendekezo moja kwa waziri mkuu Wen Jiabao nilisema, serikali inaweza kutoa uhakikisho wa maisha ya kimsingi kwa wakulima na wafugaji wa sehemu zenye matatizo ya kiuchumi au la? Waziri mkuu Wen Jiabao alikubali pendekezo langu, na kuliweka kwenye ripoti ya kazi za serikali ya mwaka ujao, ili kuanzisha utaratibu wa kuhakikisha maisha ya kimsingi vijijini kote nchini."

Ndivyo hivyo, maskani ya bibi Maria ilikuwa sehemu ya kwanza kutekeleza utaratibu wa kuhakikisha maisha ya kimsingi vijijini. Hivi sasa utaratibu huo umetekelezwa kwenye sehemu ya kati na magharibi mwa China, na katika siku za usoni utaratibu huo utatekelezwa kote nchini China.

Kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2007, Bibi Maria alitoa mapendekezo zaidi ya 50 kwenye bunge la umma la China ambayo yalizingatiwa kwa makini na kujibiwa na idara husika. Mapendekezo 7 kati ya hayo yalitolewa uso kwa uso kwa waziri mkuu Wen Jiabao na viongozi wengine wa China, hadi sasa mapendekezo manne yametekelezwa. Kutokana na kuwa yeye alifanya kazi nzuri wakati alipokuwa mjumbe wa awamu wa 10 wa bunge la umma la China na watu wanaridhika sana na kazi yake, mwaka huu alichaguliwa tena kuwa mjumbe wa mkutano wa bunge la awamu ya 11 la umma la China.

Akiwa kada wa kike wa kabila dogo, Bibi Maria alipendekeza nchi itilie maanani zaidi kuwaandaa makada wanawake hasa makada wa makabila madogomadogo, alisema:

"Makada wa makabila madogomadogo ni wachache kwenye maskani yangu, hasa makada wa wanawake. Nina matumani kuwa nchi yetu inaweza kuwaandaa makada wengi zaidi wa makabila madogomadogo wenye ujuzi wa sayansi na utamaduni, ili kuwaongoza wakulima na wafugaji kujiendeleza na kupata maisha mazuri zaidi."

Idhaa ya kiswahili 2008-03-13