Katika miaka ya hivi karibuni, maendeleo ya kasi kwenye eneo la maendeleo ya uchumi na teknolojia la Tianjin (TEDA) yameleta fursa mpya kwa shughuli za mahoteli mjini Tianjin. Hoteli ya Renaissance TEDA ya Tianjin ni hoteli kubwa zaidi ya nyota tano kwenye eneo hilo. Meneja mkuu wa hoteli hiyo ni Bw. Hans Loontiens kutoka Ubelgiji.
Kabla ya kufika Tianjin Bw. Lootiens, alikuwa meneja mkuu wa hoteli moja nchini Misri. Mwezi Novemba mwaka 2007 alituma kwenda kufanya kazi mjini Tianjin. Bw. Lootiens alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, baada ya kupata habari hiyo alianza kutafuta habari kuhusu mji wa Tianjin na eneo la maendeleo ya uchumi na teknolojia ya Tianjin. Alikuwa na matumaini makubwa kuhusu kazi yake, alisema,
"Hivi sasa vifaa na huduma za hoteli yetu ni nzuri zaidi kuliko hoteli nyingine, hivyo tuna imani kuwa hoteli yetu inaongoza kwenye eneo hilo, na tutaendelea kuinua kiwango cha huduma zetu. Ukichukua nafasi ya kwanza katika sehemu fulani, washindani wengi watajaribu kukushinda, lakini ushindani utakuhimiza kujiendeleza, na kuendelea kuhakikisha unaongoza."
Bw. Lootiens alisema baada ya kufika kwenye eneo la maendeleo ya uchumi na teknolojia la Tianjin, aliona kuwa shughuli za kiuchumi zinaendelea vizuri, na makampuni mengi kati ya makampuni 500 yenye nguvu kubwa zaidi duniani yameanzisha matawi yao huko. Mambo hayo yamempatia imani kuhusu mustakabali wa kazi yake, aliona kuwa, hoteli za nyota tano si nyingi katika sehemu hiyo, hivyo hoteli ya Renaissance TEDA ina uwezo mkubwa wa ushindani, alisema,
"Serikali inatilia mkazo maendeleo ya eneo la maendeleo ya uchumi na teknolojia la Tianjin. Kuweza kufanya kazi katika eneo hilo lenye maendeleo ya haraka ni jambo la kusisimua. Naona kuwa meneja mkuu wa hoteli katika sehemu ambayo shughuli za mahoteli inapata maendeleo mazuri kutanipatia uzoefu mkubwa wa kazi."
Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya utandawazi kwenye sehemu hiyo, eneo la maendeleo ya uchumi na teknolojia la Tianjin limekuwa eneo kubwa zaidi linaloshughulikia shughuli za nje mjini humo, ambalo wageni zaidi ya elfu 2 kutoka nchi na sehemu 33 wanaishi huko kwa muda mrefu. Bw. Lootiens anajua mambo mengi kuhusu China, na aliwahi kufanya kazi katika miji mbalimbali ukiwemo Shanghai kwa miaka zaidi ya 10, lakini alishangazwa na mabadiliko makubwa ya China yaliyotokea katika miaka zaidi ya 10 iliyopita, ambayo ni pamoja na mabadiliko ya sura za miji na utaratibu wa kufanya kazi, alisema,
"Nilifanya kazi mjini Shanghai miaka zaidi ya 10 iliyopita, utaratibu wa kupata idhini ya kuishi na kufanya kazi nchini China ilikuwa itapita utaratibu mwenye utatanishi mkubwa, lakini nilipokuja Tianjin, ilikuwa rahisi kupata idhini. Hilo ni badiliko kubwa la China. China imerahisisha utaratibu wa kutoa idhini kwa wageni wanaotaka kuishi hapa."
Alipotaja eneo la maendeleo ya uchumi na teknolojia la Tianjin, Bw. Lootiens anaona kuwa ni rahisi kuishi huko, alisema,
"Nilipoishi nchini China miaka zaidi ya 20 iliyopita, haikuwa rahisi kununua vitu nilivyotaka madukani. Lakini hivi sasa kwenye supamaketi kuna vitu vingi vinavyohitaji. Zamani kama mgeni akitaka kuishi na kufanya kazi nchini China, ilikuwa ni lazima aje na vitu mbalimbali, lakini hivi sasa hakuna haja ya kufanya hivyo."
Bw. Lootiens alisema, ingawa amefanya kazi mjini Tianjin kwa muda mfupi tu, lakini ana upendo mkubwa kuhusu China, kwa sababu mke wake ni mchina anayetoka mji wa Shanghai. Alikutana na mke wake miaka 23 iliyopita mjini Shanghai, na hivi sasa wameoana kwa miaka 21. Baada ya kuoana waliishi mjini Shanghai kwa miaka kadhaa, na baadaye kutokana na uhamisho wa kazi, walikwenda kuishi kwenye nchi mbalimbali duniani. Kutokana na maelewano na uungaji mkono wa mke wake, Bw. Lootiens anafahamu sifa ya wanawake wa China, alisema,
"Wanawake wa China wana moyo mwema, wanakubali vitu vipya na mabadiliko, si wanawake kutoka nchi zote wanaweza kuwa hivyo. Kama mtu akitaka kufanya kazi vizuri zaidi, ni lazima awe na familia yenye utulivu."
Bw. Lootiens ameishi mjini Tianjin kwa muda mfupi tu, hivyo ana hamu kubwa ya kujua habari kuhusu sehemu mbalimbali za mji huo. Anataka kutembelea sehemu ya ukuta mkuu iliyoko mjini Tianjin na mitaa ya zamani ya mji huo. Alipotaja Baozi ya Goubuli ambayo ni chakula cha jadi cha mji wa Tianjin, alifurahi sana, alisema hiki ni chakula kitamu ambacho alitamani kuonja kwa miaka zaidi ya 10 iliyopita, alisema,
"Nilikwenda kuhudhuria mkutano mjini Tianjin, nilikula Baozi ya Goubuli kwa mara ya kwanza. Katika miaka 15 iliyopita, nilikwenda Beijing na rafiki yangu. Rafiki yangu alinishauri nile chakula hicho mjini Tianjin, lakini wakati huo kutokana na ukungu mkubwa barabara ya kasi ilikuwa imefungwa kwa hiyo hatukuweza kwenda Tianjin. Na sasa nimekula chakula hicho maarufu, ninafurahi sana."
Mji wa Tianjin ni chimbuko la viwanda katika zama za karibu za China, pia ni chimbuko la michezo ya Quyi, michezo ya ngonjera, picha za mwaka mpya na opera ya kibeijing zinapendwa na wenyeji wa Tianjin, pia zinapendwa na wageni wanaokwenda huko. Bw. Lootiens anaona kuwa, utamaduni wa jadi ni roho ya mji, ana matumaini kuwa mji huo utastawisha utamaduni wa jadi, alisema,
"Wageni wanavutiwa na utamaduni wa kale wa China. Tuna matumani kuwa wachina wanapoendeleza mji wa Tianjin na nchi ya China, watahifadhi vizuri utamaduni wa kale."
Mwaka huu ni mwaka wa panya. Wachina wanauita mwaka wa panya wa dhahabu ambao unamaanisha kuwa utawapatia watu bahati nzuri. Bw. Lootiens ana matumaini kuwa kazi yake itapata maendeleo zaidi, pia amewatakia wasikilizaji wetu wapate mafanikio mwaka huu, alisema,
"Ninawatakiwa muwe na afya nzuri, mpate mafanikio kwenye kazi zenu, na kutimiza ndoto zenu katika mwaka wa panya. Katika mwaka 2008 mtakuwa na mafanikio mengi."
|