Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-03 15:43:08    
Biashara iliyostawi katika mji wa kupigia filamu na televisheni nchini China

cri

Katika miaka ya hivi karibui filamu zilizopigwa chini ya mwongoza filamu maarufu wa China Bw. Zhang Yimou zimekuwa zinajulikana duniani kutokana na filamu alioongoza, hasa filamu za "Shujaa" na "Curse of the Golden Flower". Watazamaji wa filamu hizo walivutiwa na mazingira ya mapambano makali, lakini mazingira hayo yote yalipigwa katika mji wa Hendian wa kupigia filamu na televisheni nchini China.

Mji wa kupigia filamu na televisheni uko mkoani Zhejiang. Kila mtu akiingia kwa mara ya kwanza katika mji huo atajiona kama amekuwa katika dunia kadhaa tofauti, huko mjini licha ya kuwepo kwa kumbi kubwa za kifalme, pia kuna bustani za aina ya sehemu ya kusini ya China, licha ya kuwepo kwa vijiji vidogo na barabara nyembamba zilizokuwepo katika zama za karne ya 12 na 13 nchini China, pia kuna mitaa yenye maduka mengi ya Hong Kong, mtu akitembelea mji huo anaona kama amepita karne nyingi zilizopita.

Imefahamuka kwamba tokea mwaka 1996 hadi leo mji huo kwa jumla umewekezwa Yuan bilioni 2.6, na kwa nyakati tofauti yamejengwa mazingira ya aina 13 ikiwa ni pamoja na "mitaa ya Hong Kong", "kumbi za kifalme za enzi za Ming na Qing", "kasri la mfalme wa Enzi ya Qin" na "mandhari ya mito na milima kusini mwa China". Mandhari hayo karibu yameonesha mandhari ya jamii katika historia nzima ya China. Hadi sasa mji huo wa Hengdian umekuwa kituo chenye huduma kamili kwa upigaji filamu. Naibu meneja mkuu wa mji huo Bw. Liu Rongdong alisema, hivi sasa mji huo umekuwa mji wenye huduma kamili kwa kupigia filamu na televisheni nchini China. Alisema,

"Huduma zetu kwa ajili ya kupigia filamu na televisheni ni bora kabisa nchini China, mazingira yaliyopo hapa yanaweza kukidhi mahitaji ya mazingira ya enzi mbalimbali za kihistoria, na licha ya huduma za mazingira pia tunatoa huduma nyingine za kutoa waigizaji, vifaa vya uigizaji, mavazi, taa za kuangazia, chakula, hoteli na matengenezo ya mwisho ya kukamilisha filamu."

Kutokana na huduma hizo unaweza kuingia mjini humo na maandishi ya uigizaji, na kutoka na filamu yako kamili. Vikundi vingi vya uigizaji filamu vinachagua mji huo kuwa mahali pa kupiga filamu zao. Hadi sasa michezo ya filamu na televisheni zaidi ya 400 ilipigwa hapo. Mwandishi wa habari alizungumza na kikundi kinachopigia filamu ya "Mapenzi ya Kufa na Kupona". Bw. Li Wenchang ni mkurugenazi wa matengenezo ya filamu hiyo, alisema mazingira ya filamu yake inayoeleza vita dhidi ya wavamizi wa Japan vilivyotokea katika miaka ya 30 ya karne iliyopita karibu yote yalipigwa huko. Alisema,

"Naona mji huu wa Hengdian unafaa sana kwa kupiga filamu yetu, 99% ya filamu hiyo imepigwa hapa. Tunaweza kupata waigizaji, na mazingira ni ya aina nyingi ambayo yanaweza kukidhi mazingira ya hadithi yenyewe, na gharama za kutumia mazingira hayo ni nafuu, tunaweza kuokoa pesa nyingi."

Mji wa Hengdian wa kupigia filamu na televisheni sio tu una mpango wa kuendeleza kuwa kituo kikubwa kabisa cha kupigia filamu na televisheni barani Asia, tena una mpango wa kuufanya mji huu uwe ni kivutio kikubwa cha utalii. Naibu meneja mkuu Bw. Liu Rongdong alisema hivi sasa mji huo umekuwa ukielekea kwenye kivutio kikubwa cha utalii wa aina yake. Kila baada ya filamu fulani iliyopigwa hapa kuoneshwa watalii wengi waliowahi kuangalia filamu hiyo wanakuja hapa. Alisema,

"Kwa mfano, filamu iitwayo 'Kikomo Kisicho na Mwisho' iliyopigwa hapa mwaka 2006, baada ya filamu kuoneshwa, tulioesha mazingira yaliyopigwa katika filamu hiyo, watalii waliweza kuigiza wao wenyewe katika mazingira yaliyokuwa katika filamu kwa mujibu wa maandishi ya filamu hiyo, na tuna wapigaji filamu wanaowapiga picha za video kutimiza hamu yao ya kuigiza filamu."

Hivi sasa mji wa Hengdian umekuwa kivutio cha utalii cha ngazi ya taifa. Mwaka 2007 mji huo ulipokea watalii milioni 4.8, watalii wengi na vikundi vingi vya michezo ya filamu na televisheni vilituletea biashara nyingi. Naibu meneja mkuu wa mji huo Bw. Liu Rongdong alisema,

"Bishara za mjini pia zinafanywa na wafanyabiashara binafsi, kwa mfano malazi, mikahawa, vyakula vyenye mapishi ya sehemu tofauti za China, wafanyabiashara hao pia wanaweza kuigiza. Kwa hiyo huu ni mji ambao hakuna watu wasio na ajira."

Bw. Zhang Genmiao ni mfanyabiashara wa mkahawa katika mji huo. Tokea mwaka 2002 biashara yake imekuwa ikistawi mwaka baada ya mwaka. Alisema,

"Mimi ni mwenyeji wa hapa, biashara yangu ni kuwahudumia waigizaji na watalii chakula, kwa kawaida kila siku nawahudumia chakula watu kati ya mia nane hadi elfu moja, faida si ndogo, kama nisingekuwa hapa biashara yangu haiwezi kuwa nzuri kama hivi."

Kutokana na ustawi wa shughuli za mji huo, hali ya usafiri na mazingira ya mji pia imebadilika sana, na fikra za wakazi wa sehemu hiyo pia zimekuwa zinaondana na wakati badala ya kuwa nyuma kama zamani. Wataalamu wanaona kuwa kustawisha utalii kwa kustawisha huduma bora za upigaji filamu wa michezo ya televisheni ni mfano mzuri. Lakini Bw. Liu Rongdong alisema, mwanzoni walipoanzisha mji huo walikumbwa na matatizo mengi. Alisema,

"Mwanzoni watu wengi walikuwa hawaoni mustakbali mzuri wa mji huo, tatizo moja ni hali mbaya ya usafiri. Mwanzoni safari kutoka mji wa Hangzhou, mji mkuu wa mkoa wa Zhejiang, hadi hapa, ilihitaji muda wa saa 6 hadi 7. Tatizo jingine ni kuwa hapa Hengdian ulikuwa mji wa viwanda, na kulikuwa na upungufu wa maji."

Lakini matatizo hayo hayakukwamisha maendeleo ya mji huo. Hivi sasa mji huu umekuwa na raslimali zenye thamani ya Yuan bilioni tatu, chini ya makao makuu ya kampuni kuna kampuni ya kupigia filamu za michezo, kampuni ya utalii, na maduka zaidi ya 20, watu wanaoshughulikia utalii na shughuli za upigaji filamu wako zaidi ya elfu mbili. Bw. Liu Rongdong alisema, lengo la mji huo ni kuwa baada ya juhudi za miaka kumi litafikia kiwango cha kuongoza duniani katika sekta ya kupigia filamu za michezo na utalii. Alisema,

"Baada ya miaka kumi katika huduma na mapato tutafikia kiwango cha Hollywood na Diness."

Idhaa ya kiswahili 2008-04-03