Tangu China na Mauritania zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi mwaka 1965, ingawa hali ya dunia inabadilika, lakini uhusiano na ushirikiano wa kiwenzi kati ya nchi hizo mbili unaendelea kwa utulivu, na nchi hizo mbili zimekuwa marafiki wa kutegemeana na zimefungua ukurasa mpya wa historia ya uhusiano kati ya China na Afrika.
Uhusiano wa kisiasa kati ya China na Mauritania ni imara, nchi hizo mbili zinamaoni ya pamoja au yanayolingana kuhusu masuala makubwa ya kimataifa, na zinashirikiana na kuungana mkono katika mambo ya kimataifa. Mauritania siku zote inashikilia sera ya kuwepo kwa China moja na haikuwa na uhusiano wa kiserikali kati yake na Taiwan, na kufuata msimamo wa kuunga mkono muungano wa China. Katika miaka zaidi 40 iliyopita, viongozi wa nchi hizo mbili walitembeleana mara kwa mara, Bw Abdellahi wa Mauritania aliyechaguliwa kuwa rais mwezi Machi mwaka 2007 pia alieleza matumaini yake ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya Mauritania na China. Rais Hu Jintao wa China alimpigia simu na kumpongeza Bw. Abdellahi kwa kuchaguliwa kuwa rais na kutuma mjumbe maalumu kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwake.
Uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Mauritania unaendelezwa vizuri. Mwezi Desemba mwaka 2006, pande hizo mbili zilisaini makubaliano ya Mauritania kutambua hadhi ya uchumi wa soko huria ya China na makubaliano ya serikali ya China kuipa serikali ya Mauritania ushuru wa forodha wenye unafuu. Thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili katika mwaka 2007 ilifikia dola za kimarekani milioni 707 na kuongezeka kwa asilimia 38.3 kuliko mwaka 2006 wakati kama huu. Bidhaa ilizouza China kwa Mauritania ni ngao, chai, mashine, vyombo vya umeme nyumbani, na bidhaa za teknolojia mpya ya hali ya juu, na China kuagiza bidhaa kutoka Mauritania kama vile mazao ya majini, madini ya mchanga wa chuma na mafuta ghafi.
China na Mauritania zilifanya juhudi kuanzisha ushirikiano katika sekta ya teknolojia, China ilisaidia ujenzi wa miradi 36 ikiwemo bandari ya Nouakchott, kituo cha mikutano ya kimataifa, jengo la ikulu, miradi 10 ya ushirikiano wa teknolojia na miradi 8 ya ukaguzi. Hivi sasa miradi itakayoanzishwa ni pamoja na miradi ya majengo matatu ya serikali, hospitali moja na shule mbili za kijiji. China ilianzisha ujenzi wa miradi nchini Mauritania tangu mwaka 1982. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2007, thamani ya mipango ya miradi iliyojengwa na makampuni ya China nchini Mauritania ilifikia dola za kimarekani milioni 663. Miradi hiyo ni pamoja na utoaji wa maji, usambazaji wa umeme, kushughulikia mashamba ya kilimo na ujenzi wa barabara. Makampuni ya China yamewekeza dola za kimarekani milioni 80 nchini Mauritania. Hivi sasa makampuni ya China yaliyowekeza nchini Mauritania ni pamoja na kampuni ya miradi ya nje ya China, kampuni ya Luqiao ya China, kampuni ya uuzaji na uagizaji wa vyombo ya China, kampuni ya miradi ya kimataifa ya Zhongdi, kampuni ya Zhongxing, kampuni ya Huawei, kampuni ya mazao ya majini ya China na kampuni ya mazao ya majini ya Shanghai.
Katika sekta ya utamaduni, nchi hizo mbili zilisaini makubaliano ya ushirikiano wa utamaduni mwaka 1967. China imekuwa inatoa misaada ya udhamini wa masomo kwa Mauritania kuanzia mwaka 1975, hadi kufikia mwaka 2007 imepokea wanafunzi 140 waliopata udhamini wa masomo. Kutokana na maendeleo ya uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya China na Mauritania, watu wa Mauritania wanaongeza hamu ya kujifunza Kichina siku hadi siku. Aidha madaktari wa China wanatoa mchango mkubwa nchini Mauritania na kusifiwa na wananchi wa Mauritania.
Habari nyingine zinasema, katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na viongozi wa China na Morocco kutembeleana mara kwa mara, ushirikiano wa kirafiki na kijadi kati ya nchi hizo mbili ulifungua ukurasa mpya, na uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelezwa kwa kina siku hadi siku kwenye kiwango cha juu zaidi, ushirikiano katika sekta mbalimbali unaongezeka na mawasiliano katika ngazi mbalimbali yanaendelea vizuri.
Balozi wa China nchini Morocco Bw. Gong Yuanxing alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema, baada ya mfalme Mohamed wa sita wa Morocco kuzuru China kwa mara ya kwanza mwaka 2002, rais Hu Jintao wa China aliizuru Morocco mwaka 2006, baadaye viongozi wa pande hizo mbili walitembeleana mara kwa mara, na uhusiano wa kisiasa uliimarishwa. Morocco siku zote inashikilia sera ya kuwepo kwa China moja na kutofanya mawasiliano yoyote ya kiserikali na Taiwan. China na Morocco zinashirikiana vizuri na kuungana mkono katika mambo ya kimataifa. Utaratibu wa mazungumzo ya kisiasa ya wizara za mambo ya nje za nchi hizo mbili ulianzishwa mwaka 2007 na unatekelezwa vizuri.
Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara ni sehemu muhimu ya uhusiano kati ya China na Morocco. Mwaka 2007 thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili ilifikia dola za kimarekani bilioni 2.584. Tangu mwaka 2002, biashara ya pande mbili kati ya China na Morocco inaongezeka kwa 20% na kasi ya ongezeko hilo kwa mwaka 2007 ilifikia 34%. Na ili kuisadia Morocco kupunguza pengo la biashara kati yake na China, China inafanya juhudi kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka Morocco.
Tangu mwaka 1988 China na Morocco zishirikiane kuunda kampuni ya uvuvi, ushirikiano wa kunufaishana kati yao umeendelea kwa miaka 20. Hivi sasa makampuni ya China yenye uwezo mkubwa, yamejiwekea msingi thabiti katika soko la mradi ya ujenzi nchini Morocco, vyombo vya mawasiliano ya habari vilivyotengenezwa na China vinatumiwa katika mfumo wa mawasiliano ya tayari ya Morocco, magari yaliyotengenezwa na China yanauzwa vizuri nchini Morocco. Bw. Gong Yuanxing alisema hali ya kisiasa ya Morocco ni ya utulivu, uchumi wake unaendelezwa vizuri, na ameyataka makampuni ya China yaende Morocco kuwekeza na kuongeza nguvu mpya kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Morocco ni nchi ambayo China imetuma vikundi vingi kabisa vya madaktari. Tangu mwaka 1975 hadi sasa, mji wa Shanghai ulituma vikundi zaidi ya 120 vilivyoundwa na madaktari zaidi 1,300 nchini Morocco, hivi sasa madaktari 121 wanaishi kwenye sehemu za mbali za Morocco, wanafanya kazi kwa bidii na kuwasaidia wananchi wa huko kupunguza maumivu ya ugonjwa na kueneza urafiki. Tarehe 1 mwezi Novemba mwaka 2008, China na Morocco zitaadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati yao. Katika nusu ya karne iliyopita, kutokana na juhudi za viongozi wa nchi hizo mbili, urafiki kati ya China na Morocco umekuwa na mafanikio makubwa. Tunaamini kuwa katika siku za baadaye, uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili utaimarishwa zaidi.
Wasikilizaji wapendwa, kufikia hapo ndiyo kwa leo tunakamilisha kipindi hiki cha daraja la urafiki kati ya China na Afrika, kwa herini.
|