Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-07 15:45:04    
Tarafa maarufu ya Boao, mkoani Hainan China

cri

Kwenye pwani ya mashariki ya bahari ya kusini ya China kuna tarafa moja ndoto iitwayo Boao, tarafa hiyo ina eneo la kilomita za mraba 2 tu pamoja na watu elfu 10. Tokea mwaka 2002, kila mwaka mkutano wa baraza la Asia la Boao unafanyika huko. Kila ifikapo wakati huo, tarafa hiyo ndogo inafuatiliwa na vyombo vya habari vya duniani. Boao iko mjini Qionghai, mkoani Hainan, China, mfanyakazi wa serikali ya mji Bw. Wang Yi alishiriki kwenye kazi za mwanzoni mwa maandalizi ya uanzishwaji wa baraza la Boao. Alisema mwaka ule ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika huko kutoka mjini, hali aliyoiona ilimfanya akumbuke makala maarufu ya "Taohuayuanji" iliyoandikwa na mshairi wa kale wa China, Tao Yuanming. Alisema

"Mwaka 1985 nilifika kwenye tarafa ya Boao, halafu nilikwenda kwenye kisiwa cha Dong Yu kwa mashua, njiani niliwaza, hapa ndipo Taohuayuan, kisiwa kizima cha Dong Yu ni kizuri kama Xanadu, hususan wanakijiji wa hapa ni wapole na wema kabisa."

Mandhari hiyo nzuri ya kimaumbile ilimvutia Bw. Jiang Xiaosong, ambaye ni mwanakiwanda na mtu maarufu katika jamii, aliamua kuanzisha kampuni kwenye sehemu ya Boao na kuiendeleza sehemu hiyo. Baada ya hapo Bw. Jiang Xiaosong akitumia athari zake, aliwaalika viongozi wa zamani wa serikali za nchi tatu za Japan, Australia na Philippines kucheza mchezo wa golf huko, hatimaye walitoa pendekezo la kuanzisha baraza la kudumu la Asia la Boao. Mwezi Februari mwaka 2001, baraza la Asia la Boao lilianzishwa rasmi kwenye sehemu ya Boao. Kutokea mwaka wa pili, mkutano mkuu wa baraza hilo umekuwa unafanyika huko kila mwaka katika mwezi Aprili, viongozi wa siasa wanakwenda huko kuhudhuria mikutano mbalimbali na kujadili masuala makubwa ya sehemu ya Asia na Pasifiki pamoja na ya dunia nzima.

"Nilikwenda Boao bila kutarajia, nilishangazwa na mandhari nzuri ya huko, nikajiwa na wazo la kuiendeleza. Boao haikuchaguliwa kutokana na kuweko kwa baraza la Asia, bali ni kuwa baraza la Asia liliundwa kutokana na kuweko kwa Boao. Ni dhahiri kuwa kuundwa baraza la Asia ni kutokana na mahitaji makubwa ya Asia kwa wakati ule."

Ni mwendo wa nusu saa hivi kwa gari kufika tarafa ya Boao kutoka mjini. Barabara nyingi zimeunganisha Boao na sehemu nyingine. Tokea mwanzoni mwa karne hii hadi hivi sasa, idadi ya wakazi wa tarafa hiyo imeongezeka karibu kwa mara kumi, muundo wa uchumi wa zamani uliotegemea kilimo na uvuvi umebadilika kutegemea zaidi sekta ya utalii. Sasa zaidi ya 60% ya watu wa huko wanashughulikia kazi zinazohusika na utalii. Mikutano inayofanyika huko kila mwaka inazidi 100. Licha ya hayo, hoteli mbalimbali za ngazi ya nyota pia zimeongezeka kwa haraka, na hoteli zile zilizoanzishwa na wakulima wa huko zimefikia 35, na idadi ya watalii waliofika huko inafikia milioni 2 au 3 hivi. Shamrashamra zinaonekana zaidi kwenye magati ya pwani ya Yudai ya tarafa ya Boao, hususan katika majira ya utalii.

Mwongoza watalii wa shirika la utalii la Hainan, Bw. Wang alisema, kwa wastani kila mwezi anayatembeza makundi manne ya watalii, ambapo kivutio kikubwa zaidi kwa watalii hao ni mandhari nzuri ya maumbile. Alisema,

"Kufika Boao, hasa ni kwa ajili ya kuangalia mandhari ya maumbile, mandhari ya hapa ni yenye umaalumu wa kipekee kwenye mkoa wa Hainan, hapa kuna makutano ya mito mitatu, pwani ya Yudai, ambayo ni nyembamba zaidi ya duniani, na ni nadra kupatikana, sababu muhimu ya kufanyika kwa mikutano ya baraza la Asia la Boao ni kutokana na mandhari nzuri ya kuvutia ya huko."

Zaidi ya miaka minane iliyopita, Bw. Fu Zhifu alikuwa anajishughulisha na uvuvi kwenye sehemu ya mwanzo ya mto Wanquan, halafu aliingia kwenye sekta ya utalii. Kila siku aliwapeleka watalii kutoka kwenye gati lake hadi kwenye kisiwa cha Dong Yu na pwani ya Yudai. Alisema, shughuli zake za utalii zimeendelezwa vizuri sana, hivi sasa idadi ya watalii wa nchini na wa nchi za nje inaongezeka kwa haraka. Alisema,

"Katika gati letu hilo peke yake kuna mashua zaidi ya 50. Tuna mashua moja kubwa yenye viti 100, mashua mbili zenye viti 60 kila moja, mashua nne zenye viti 50 kila moja, tena tuna mashua kadhaa kwa ajili ya wageni maalumu wakiwemo wanaokuja kuhudhuria mikutano. Ikiwa kuna wageni wengi, kila siku tunafanya safari zaidi ya 10 au zaidi ya 20."

Wakazi wa Boao ni wapole na wachangamfu. Bw. Huang Dunji mwenye umri wa miaka 63 ameendesha shughuli za duka la kuoka bata mzinga kwa zaidi ya miaka 20, duka lake ni maarufu sana katika sehemu hiyo. Zamani duka lake lilikuwa dogo sana, ambalo lilitembelewa na wakazi wa tarafa hiyo kwa ajili ya chakula na mazungumzo. Sasa duka lake limeendelezwa kuwa nyumba kubwa la ghorofa yenye mita za mraba zaidi ya 300, watalii wa nchini na wa nchi za nje pia wanakwenda huko mara kwa mara.

"Vitoweo vinavyopikwa na duka letu ni vizuri sana, hivyo tumepata wateja wengi. Mke wangu ni hodari sana wa kupika vitoweo vya wenyeji. Tunajitahidi kuwaridhisha wageni, wakifurahi, watafika tena kwenye duka letu tena."

Katika siku ambapo mikutano hiyo miwili muhimu inapofanyika, watalii wengi hutembelea Boao wakati wa asubuhi. Wakazi wanaoendesha mashua, shughuli za kusafisha picha za studio na wanaouza mazao maalumu ya huko hurudi nyumbani saa nane au saa tisa mchana hivi. Wakati huo tarafa hiyo ndogo hurejea katika hali ya shwari. Watu wachache tu wanatembea barabarani.

Katibu wa kamti ya chama ya tarafa ya Boao Bw. Wu Enze alisema, katika mpango wa maendeleo wa siku za baadaye, tarafa ya Boao itazungukwa na eneo maalumu la maendeleo lenye kilomita za mraba zaidi ya 100, uwezo wa kutoa huduma na usimamizi wa kitaalamu wa tarafa hiyo utainuka zaidi. Tumaini lake ni kujenga tarafa hiyo kuwa mahali pazuri kabisa pa utalii na mapumziko. Alisema,

"Tumetoa wito wa kujenga tarafa yetu kuwa mahali pazuri kabisa, kwani tuna mabingwa wengi wa mambo ya utalii na utamaduni, sisi hatutaijenga kuwa mji, hapa ni tarafa ndogo, tutaijenga kuwa tarafa nzuri kabisa na tarafa yenye umaalumu wa utulivu, shwari, neema, ya kuvutia na mahali pazuri pa kuishi, tutawavutia wakazi wa mijini waje hapa kupumzika, na wajiburudishe na maisha ya hapa."

Idhaa ya kiswahili 2008-04-07