Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-04-16 16:14:01    
Wataalamu wapendekeza watu wachukue tahadhari kuhusu magonjwa ya figo

cri

Magonjwa ya figo ni magonjwa yanayotokea mara kwa mara na kusababisha vifo vya wagonjwa wengi, lakini watu hupatwa na magonjwa hayo bila dalili dhahiri, na watu wengi wanaopatwa na magonjwa hayo huenda hawajigundui. Wataalamu wanasema kugunduliwa mapema na kuweka kinga dhidi ya magonjwa hayo ni mbinu zenye ufanisi zaidi za kujikinga na magonjwa magumu ya figo. Hivi sasa hali ya kinga na tiba ya magonjwa hayo nchini China bado ni mbaya, watu wanapaswa kuinua tahadhari kuhusu magonjwa hao.

Figo ni kiungo muhimu mwilini mwa mtu, si kama tu yanaondoa vitu vichafu na vyenye sumu kutoka mwilini, bali pia inarekebisha shinikizo la damu na uwiano wa hali ya ndani ya mwili. Figo pia inafanya kazi muhimu kuhakikisha uwezo wa damu na mifupa. Mkurugenzi wa idara ya magonjwa makubwa katika wizara ya afya ya China Bw. Li Xun alisema, hivi sasa magonjwa makubwa ya figo yanazidi kutokea kote duniani. Kutokana na kuboreka kwa hali ya maisha na kazi, tabia za maisha ya watu vimekuwa na mabadiliko yasiyofaa, kama vile matumizi ya baadhi ya lishe kupita kiasi, shinikizo kubwa, kutopata usingizi wa kutosha, uvutaji sigara, unywaji wa pombe nyingi pamoja na kuongezeka kwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu, na matumizi ovyo ya dawa. Tabia hizo zote zinaweza kusababisha magonjwa ya figo. Bw. Li Xun alisema:

"tunajisikia wazi madhara makubwa ya magonjwa magumu ya figo na changamoto zake zinazotukabili katika pande mbalimbali. Magonjwa hayo yamekuwa aina moja ya magonjwa makubwa yanayotishia vibaya usalama wa afya ya binadamu baada ya magonjwa ya mishipa ya damu kwenye moyo, saratani na kisukari, na yamekuwa suala la afya ya umma duniani."

Hali ya magonjwa hayo nchini China pia si nzuri. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na idara husika za China, asilimia 18.7 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 40 nchini China wanapatwa magonjwa hayo. Katibu mkuu wa idara ya magonjwa ya figo katika shirikisho la madaktari la China Profesa Zhang Youkang alisema:

"hali ya magonjwa ya figo nchini China ni mbaya, inakadiriwa kuwa watu waliopatwa na magonjwa magumu ya figo nchini China inachukua asilimia 10 ya idadi ya watu wote, na asilimia 10 tu wa watu wa China wanafahamu magonjwa hao."

Profesa Zheng Falei wa hospitali ya Xiehe ya Beijing anaona kuwa, watu wa kawaida wa China hawana ufahamu wa kutosha kuhusu magonjwa hayo, hata baadhi ya watumishi wa huduma za afya katika ngazi za msingi hawayafahamu. Wagonjwa wengi wanatafuta matibabu baada ya kuwa dalili za magonjwa hayo zimeonekana kidhahiri na yameleta madhara makubwa kwa afya yao. Profesa Zheng Falei alisema, ingawa magonjwa makubwa ya figo yanaendelea bila dalili dhahiri, lakini kama watu wakichukua tahadhari wanaweza kugundua dalili kadhaa za magonjwa hayo. Bw. Zheng Falei alisema:

"katika kipindi cha mwanzo cha magonjwa hayo, dalili hazionekani kidhahiri, lakini yakiendelea zaidi, baadhi ya dalili zinaanza kutokea, kama vile kujisikia kupungukiwa nguvu, kukosa hamu ya kula chakula, usingizi mbaya na baadhi ya watu wanaweza kugundua miguu yao inavimba, hizo zote ni dalili za kipindi cha mwanzo."

Profesa Zheng Falei pia alisema, ni vigumu kutambua magonjwa ya figo kwa kutegemea dalili hizo tu, kwa hiyo upimaji ni muhimu sana, watu wenye umri zaidi ya miaka 40 wanapaswa kufanyiwa upimaji kuhusu mkojo na uwezo wa figo kila mwaka, wagonjwa wa shinikizo la damu na kisukari wanapaswa kufanyiwa upimaji mara zaidi ya mbili kila mwaka. Bw. Zheng Faxin pia alitaja suala linaloweza kupuuzwa katika maisha ya kila siku. Baadhi ya watu wakiwa na pilikapilika za kazi, husahau kunywa maji, hata wanajizuia mara kwa mara kwenda msalani, wataalamu wanaona kuwa hii ni tabia mbaya kwa afya na figo.

Wataalamu pia wanasema, hata kama ukipatwa na magonjwa hayo huna haja ya kuwa na mahangaiko. Hivi sasa magonjwa mengi magumu ya figo yanaweza kutibiwa kwa ufanisi, ingawa ni vigumu kutibiwa kikamilifu, lakini maendeleo ya magonjwa hayo yanaweza kuahirishwa hata kusimamishwa kwa njia ya matibabu na kuacha baadhi ya mienendo ya maisha, hatua hizo zinaweza kuzuia kwa ufanisi kasi ya uwezo wa figo ya wagonjwa kuzidi kuwa mbaya na kuhakikisha usalama wa maisha yao na kupunguza matumizi ya raslimali nyingi za matibabu na gharama kwa familia na jamii. Bw. Zheng Falei alisema:

"tunaposema magonjwa ya figo ni makubwa kama wauaji wa sirisiri, maana yake ni kwamba magonjwa hayo yanaweza kusababisha madhara makubwa katika kipindi chake cha mwisho. Lakini kutokana na kuwa kipindi cha mwanzo hadi cha mwisho kinachukua muda mrefu, ingawa mchakato huo hauonekani kwa urahisi. Kama magonjwa hayo yanagunduliwa mapema na kuchukuliwa hatua mwafaka, yanaweza kudhibitiwa vizuri, wagonjwa wanaweza kuishi na kufanya kazi kama watu wa kawaida."