China na Afrika ni marafiki mazuri wa kutegemeana, zinaelewana, kuheshimiana, kuungana mkono katika mambo mengi ya kimataifa, ambazo ni mfano bora wa ushirikiano wa kusini na kusini katika uhusiano wa kimataifa. Baada ya kuingia katika karne mpya, mawasiliano kati ya viongozi wa China na nchi za Afrika na ushirikiano katika mambo ya kimataifa unaendelea kuimarishwa, mfumo wa majadiliano ya kisiasa umezidi kuwa aina mbalimbali, baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika lililoanzishwa mwaka 2000 lilianzisha mfumo wa majadiliano ya pande mbalimbali kati ya China na nchi za Afrika, na kutia nguvu mpya kwa uhusiano kati ya China na Afrika.
China inaihitaji Afrika, maneno hayo si matupu, ni halisi. Baada ya vita vya baridi, hadhi ya kisiasa ya Afrika ingawa ilielekea kuporomoka, lakini hadhi na umuhimu wake katika mikakati ya kidiplomasia ya China havikubadilika. Ingawa nchi za Afrika ni maskini, lakini kuna nchi nyingi na hali zake na misimamo yao inafanna, katika diplomasia ya pande mbalimbali, moyo wa uungaji mkono ni muhimu sana. China inahitaji uungaji mkono wa nchi za Afrika, na imepata uungaji mkono wa nchi za Afrika katika masuala ya Taiwan, Tibet, kujiunga na WTO, kuomba nafasi ya kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki, kuomba nafasi ya kuwa mwenyeji wa maonesho ya kimataifa na mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Afrika siku zote ni sehemu muhimu ya kufanya shughuli za kidiplomasia kwa China. Nchi 53 za Afrika, hasa nchi 47 zilizoanzisha uhusiano wa kibalozi na China zimepanua maeneo ya kufanya shughuli kwa China katika jukwaa la kimataifa. Historia imethibitisha kuwa, nchi za Afrika ni rafiki wa dhati wa China, kuendeleza uhusiano kati ya China na Afrika kuna umuhimu wa kimkakati katika kuinua athari ya China duniani na kuimarisha msimamo wa kidiplomasia wa China.
Hivi sasa hali ya kisiasa ya kimataifa inabadilika mara kwa mara na uchumi unaelekea kuwa wa utandawazi, nchi za Afrika zinatilia maanani hadhi na umuhimu wa China kwa ajili ya kuondoa mgogoro wa umaskini na kuwekwa ukingoni, na zinataka kupata msaada na uungaji mkono wa China. Kwa kuwa mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, China inasimama kwenye upande wa nchi za Afrika na kuunga mkono maombi na mapendekezo yanayofaa. Katika miaka ya hivi karibuni, maelewano na ushirikiano kati ya China na Afrika yanaendelea kuimarishwa, China inajibu mapendekezo ya nchi za Afrika katika masuala makubwa ya kimataifa, na kusisitiza mageuzi ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kutilia maanani suala la maendeleo na kuongeza uwakilishi wa Afrika katika mageuzi hayo na kuunga mkono pendekezo la Afrika kuhusu pande mbalimbali. Aidha China inaunga mkono juhudi za nchi za Afrika kutafuta kujiendeleza na Umoja wa Afrika kutatua masuala ya Afrika, na ilifanya juhudi kushiriki kwenye harakati ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa barani Afrika na kwenye majadiliano yanayohusiana na mambo ya Afrika. Kuanzia mwaka 1990, China ilituma askari 3,000 kwa ujumla kwenda Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Liberia na nchi nyingine za Afrika kutekeleza kazi za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Na ili kuzisaidia nchi za Afrika kutekeleza mpango wa kuendeleza rafiki mpya wa Afrika, China iliongzeza msaada wa kiuchumi kwa Afrika na kupunguza au kusamehe madeni ya nchi za Afrika, na kuzisaidia nchi za Afrika kutatua matatizo yanayozikabili katika kufungua soko, kutoa mafunzo kwa watu, kinga ya magonjwa na uhifadhi wa mazingira.
China na Afrika zinatafuta maendeleo kwa njia ya amani na pia ni nguvu thabiti za kulinda amani na utulivu wa dunia. Hivi sasa ushirikiano na uhusiano kati ya China na Afrika katika shughuli za kimataifa zinaelekea kwenye mwelekeo kazi halisi, aina mbalimbali na ya kimfumo. Waraka wa sera za China kwa Afrika uliotolewa na serikali ya China mwezi Januari mwaka huu ulipanga mwelekeo wa kuendeleza ushirikiano wa kirafiki kati yao kwenye sekta muhimu katika kipindi kipya na kutangaza China inapenda kuanzisha na kuendeleza uhusiano wa kirafiki na kimkakati wa aina mpya, uhusiano huo unalingana na mahitaji ya kipindi hiki cha amani na maendeleo, na pia unalingana na maslahi ya kimsingi ya watu wa China na Afrika na watu wa dunia, na utasaidia kujenga utaratibu wa uwiano, utulivu na masikilizano wa kimataifa.
Habari nyingine zinasema mwenyekiti wa chama cha umma cha Togo Bw. Solitoki Esso ambaye alimaliza ziara yake nchini China hivi karibuni, alisifu sana mafanikio yaliyopatikana nchini China katika ujenzi wa uchumi, hasa mradi wa magenge matatu na mabadiliko makubwa ya miji ya Beijing na Shanghai. Bw. Esso alisema kuna uhusiano mzuri kati ya chama cha kikomunisti cha China na chama cha umma cha Togo na nchi hizo mbili. Ujumbe wa Togo ulioongozwa naye ulikaribishwa vizuri nchini China. Alisema kabla ya miaka kumi iliyopita aliwahi kuzuru China, lakini mara hii alitembelea China tena, hakuweza kuzikumbuka sehemu alizotembelea kwa sababu maendeleo na mabadiliko ya China ni makubwa sana.
Habari nyingine zinasema sherehe kubwa ya kufunguliwa kwa chuo cha Confucius kwenye chuo kikuu cha Mto Suez nchini Misri. Balozi wa China nchini Misri Bw. Wu Chunhua alisema kwenye sherehe hiyo kuwa, kutokana na kuendelea kwa mageuzi na kufungua mlango na kukua kwa kasi kwa uchumi wa China, lugha ya kichina inaendelezwa kwa haraka duniani. Kuanzisha chuo cha Confucius kwenye chuo kikuu cha Mto Suez nchini Misri kunaonesha Misri kutilia maanani mafunzo ya lugha ya kichina na mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Misri, na kunakidhi mahitaji ya kuelewa utamaduni wa China, na kuna umuhimu mkubwa katika kuhimiza mafunzo ya utamaduni na lugha ya China kwenye sehemu ya kaskazini mashariki mwa Misri na kuanzisha utafiti wa China ya kisasa.
Mkuu wa chuo kikuu cha Mto Suez Bw. Mohamod Zohabi alisema kuwa kujifunza lugha ya kichina na utamaduni wa China kunasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika utamaduni, uchumi na biashara. Kuanzisha chuo hicho ni mfano wa urafiki kati ya China na Misri na chuo hicho kitakuwa dirisha la kuelewa utamaduni na lugha ya China kwa watu wa Misri. Kwenye sherehe hiyo Bw. Wu Chunhua alikabidhi vitabu vya kichina na vyombo vya mafunzo kwa chuo hicho kwa niaba ya ubalozi wa China nchini Misri.
Idhaa ya kiswahili 2008-04-18
|