Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-01 20:21:23    
Nyimbo anazoimba Han Lei

cri

Mwimbaji Bw. Han Lei alizaliwa mjini Beijing, alianza kujifunza kupiga tarumbeta (trombo), na kuanzia hapo alianza kujihusisha muziki maishani mwake. Mwaka 1999 alishiriki kwenye "mashindano ya waimbaji chipukizi" na aliwavutia wasikilizaji kwa sauti yake.

Mliosikia ni wimbo uitwao "kusafiri kila pembe la dunia". Katika miaka ya 90 ya karne iliyopita wimbo huo ulienea kote nchini China. Wimbo huu unasema, "nasafirisafiri nikipita kijiji baada ya kijiji, jua linazama na kuchomoza, dunia inazungukazunguka mwaka hadi mwaka."

Mliosikia ni wimbo wa "kusafiri kila pembe ya dunia"

Mwaka 1997 Bw. Han Lei alitoa albamu yake ya kwanza ambayo imekusanya nyimbo zake zenye mitindo tofauti. Ufuatao ni wimbo mmoja uliopo kwenye albamu hiyo uitwao "Nimkabidhi nani mapenzi na usumbufu wangu?"

Mliosikia ni wimbo alioimba Bw. Han Lei uitwao "Nimkabidhi nani mapenzi na usumbufu wangu?"

Sauti ya Bw. Han Lei ni nene na papa, ikiwa na mvuto wa kiume, anaweza kuimba nyimbo za kienyeji za China na pia nyimbo za aina ya Jazz, ni mmoja wa waimbaji wanaume wanaopendwa sana na mashabiki wa muziki wa China. Aliwahi kuimba kwa ajili ya michezo ya filamu na televisheni karibu mia moja.

Miliosikia ni wimbo alioimba kwa ajili ya filamu ya "Mfalme Han Wu". Filamu hiyo inaeleza maisha ya mfalme huyo aliyezaliwa mwaka 156 K.K. na kufariki mwaka 87 K.K. ambaye alikuwa shupavu katika enzi yake, na kuifanya miaka ya utawala wake kuwa kipindi kinachosifiwa sana katika historia ya China.

Wimbo huo unasema, "Ndani ya mto wenye maji yanayokwenda kasi, na wewe ni povu la mawimbi, na kwenye mlima unaotambaa mbali wewe ni kilele cha ajabu, wewe unajiunguza ili kuleta joto kwenye ardhi yako, miale ya moto inachezacheza kama unavyojieleza mara ya mwisho."

Idhaa ya kiswahili 2008-05-01