Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-05-27 18:16:48    
Makampuni ya China yanayouza bidhaa nje yafanya juhudi kukabiliana na matatizo ya biashara na nje

cri

Tarehe 30 mwezi Aprili maonesho ya 103 ya bidhaa za China zinazouzwa nchi za nje yalifunguliwa mjini Guangzhou. Hivi sasa kutokana na msukosuko wa mikopo ya ngazi ya pili uliotokea nchini Marekani, na kupanda kwa thamani ya fedha ya China renminbi, biashara ya China na nje inakabiliwa na hali ya wasiwasi zaidi, hivyo maonesho ya bidhaa za China zinazouzwa katika nchi za nje ambayo yanaonesha hali ya biashara ya China na nje yanafuatiliwa na watu wengi. Kwenye maonesho hayo, mwandishi wetu wa habari alifahamishwa kuwa, makampuni ya China yanafanya juhudi kubadilisha miundo ya bidhaa zinazouzwa nje ili kukabiliana na matatizo ya biashara na nje.

Maonesho ya bidhaa za China zinazouzwa nchi za nje yanafanyika kila baada ya miaka miwili. Hayo ni maonesho ya kimataifa ya bidhaa ambayo ni makubwa zaidi nchini China na yamefanyika kwa muda mrefu zaidi na kupata mafanikio makubwa zaidi. Tarehe 30 mwezi Aprili maonesho ya 103 ya bidhaa za China zinazouzwa nchi za nje yalifunguliwa mjini Guangzhou. Kwenye maonesho hayo, wafanyabiashara mbalimbali walipohojiwa na mwandishi wa habari walisema,

"Makubaliano miwili ya kuagiza bidhaa ya Uturuki yalifutwa, ni wazi kuwa hali ya biashara ni ya wasiwasi. Hivi sasa hakuna utaratibu wa kurudisha ushuru, thamani ya renminbi inapanda, bila shaka bei za bidhaa kwa dola za Kimarekani zitapanda. Wateja kutoka nje hawawezi kukubali bei hizo."

"Hivi sasa kutokana na kubadilika kwa kiwango cha ubadilishaji wa fedha za Renminbi kwa fedha za kigeni, kupanda kwa thamani ya fedha za Renminbi, na kupanda kwa gharama za uzalishaji, makampuni yamekuwa yanakabiliwa na matatizo."

Maonesho ya bidhaa za China zinazouzwa nchi za nje yametoa ishara ya onyo kwa makampuni yanayouza bidhaa nje kuwa ongezeko la uuzaji wa bidhaa mbalimbali linaelekea kupungua. Takwimu kutoka idara kuu ya forodha ya China zinaonesha kuwa, katika robo ya kwanza ya mwaka huu thamani ya uuzaji wa bidhaa za China katika nchi za nje ilikuwa dola za kimarekani bilioni 300, ongezeko hilo lilipungua kwa ailimia 5 kuliko mwaka jana wakati kama huu, na urari wa biashara na nje ulipungua kwa asilimia 11 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

Wafanyabiashara wengi wanaouza bidhaa katika nchi za nje wanasema, kupanda kwa thamani ya fedha ya renminbi kumekuwa shinikizo kubwa kwao, kwani kumepunguza faida za makampuni ambayo bei za bidhaa zake zilikuwa zinapangwa kwa kutumia dola ya kimarekani. Makampuni yanayotegemea kuuza bidhaa zake katika nchi za nje yakiwemo makampuni ya nguo yameathiriwa zaidi. Meneja mkuu wa kampuni ya nguo ya kimataifa ya Zhongfang Bw. Li Lingmin alisema,

"Wakati tuliposaini makubaliano mwishoni mwa mwaka jana, kiwango cha ubadilishaji wa fedha za Renminbi kwa dola za Kimarekani kilikuwa yuan 7.2 kwa dola ya Kimarekani 1, lakini tutakapotekeleza makubaiano hayo mwezi Juni mwaka huu, kiwango cha ubadilishaji wa fedha za Renminbi kwa dola za Kimarekani kitakuwa yuan 6.8 hivi kwa dola za Kimarekani 1. Hivyo tuliposaini makubaliano, tulifikiri tutapata faida, lakini tutakapotekeleza makubaliano hayo tutapata hasara."

Licha ya suala la kiwango cha ubadilishaji wa Renminbi kwa fedha za kigeni, kutokana na kuongezeka kwa urari wa biashara ya China na nje, biashara ya utengenezaji wa bidhaa ambayo ilihimizwa zamani imeanza kupungua nchini China. China inaanza kutekeleza sera za kuboresha miundo ya bidhaa zinazouzwa katika nchi za nje, kuhimiza makampuni kubadilisha biashara ya utengenezaji wa bidhaa, na kudhibiti uuzaji wa bidhaa ambazo zinatumia nishati kwa wingi na kusababisha uchafuzi wakati wa uzalishaji na uuzaji wa maliasili katika nchi za nje. Aidha kupungua au kufutwa kwa utaratibu wa kurudisha ushuru, kupanda kwa bei za maliasili na gharama za kuajiri nguvu kazi, na mabadiliko mengine yaliyotokea kwenye masoko ya kimataifa ambayo yaliyosababishwa na msukosuko wa mikopo ya ngazi ya pili uliotokea nchini Marekani kumeathiri makampuni mengi ya China. Kwa mfano kwenye maonesho ya bidhaa za China zinazouzwa nchi za nje ya mwaka huu, wafanyabiashara wa nchi zilizoendelea zikiwemo nchi za Ulaya na Marekani walipungua kuliko mwaka jana.

Waziri wa biashara wa China Bw. Chen Deming alipotembelea maonesho hayo alisema wazi kuwa, hivi sasa biashara ya China na nje bado iko kwenye hali ya kawaida. Wizara ya biashara ya China siku zote inafuatilia mwelekeo wa biashara ya China na nje. Hivi karibuni wizara hiyo imetuma watu kufanya utafiti katika mikoa mbalimbali ya pwani, ili kujua hali ya uuzaji wa bidhaa nje ya makampuni mbalimbali. Wakati maonesho hayo yalipofanyika, wizara hiyo ilifanya makongamano na wajumbe wa makampuni yaliyoshiriki kwenye maonesho hayo ili kupata habari nyingi kuhusu hali hiyo.

Kupandisha bei ya bidhaa ni njia ya moja kwa moja inayochukuliwa na makampuni mbalimbali ili kukabiliana na hali ya wasiwasi. Mfanyabiashara wa nguo kutoka Marekani Bw. Jeffery Hochster anashiriki kwenye maonesho hayo mjini Guangzhou mara kwa mara, anaona kuwa bei za bidhaa zimebadilika, alisema,

"Kuanzia mwezi Desemba mwaka jana au mwezi Januari mwaka huu, bei za bidhaa zilipanda, ambazo ziliongezeka kwa asilimia 15 hadi asilimia 25 hivi."

Kupandisha bei ya bidhaa si njia nzuri zaidi ya kutatua matatizo. Makampuni mengi ya China yamechukua hatua kutengeneza bidhaa za aina mpya ili kupata masoko mapya, au kuanzisha chapa maarufu kwa kujitegemea na kupata hakimiliki kwa kujiendeleza. Meneja mkuu wa kampuni ya kutengeneza mashine ya Zhouyi ya mji wa Wuyi mkoani Zhejiang Bw. Ma Rufei alisema,

"Kila ifikapo mwanzoni mwa mwaka, tunaandaa mipango ya kutengeneza bidhaa za aina mpya. Ni vigumu kwa wateja kukubali mabadiliko ya bei za bidhaa za aina za zamani, lakini ni rahisi kukubali bei za bidhaa mpya. Faida ya mauzo ya bidhaa mpya ni nyingi kuliko bidhaa za zamani. Utengenezaji wa bidhaa za aina mpya unaweza kuongeza mahitaji ya bidhaa masokoni, na kuhimiza maendeleo ya kampuni yetu.