Mahitaji
Nyama ya kuku gramu 350, matango gramu 50, pilipili hoho gramu 5, chumvi gramu 2, chembechembe za pilipili manga gramu 1, chembechembe za kukoleza ladha gramu 1, vipande vya vitunguu maji gramu 5, tangawizi gramu 4, vitunguu saumu gramu 4, wanga gramu 10, sukari gramu 5, siki gramu 2, na ute wa yai moja
Njia
1. kata nyama ya kuku iwe vipande, changanya na chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, mvinyo wa kupikia, wanga na ute.
2. kata tango na pilipili hoho ziwe vipande.
3. koroga chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, mvinyo wa kupikia, sukari, chembechembe za pilipili manga na wanga kuwa sosi.
4. washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya nyama ya kuku, korogakoroga, tia vipande vya vitunguu maji, tangawizi na vitunguu saumu, pilipili hoho na tango, korogakoroga, mimina sosi iliyokorogwa, korogakoroga, mimina siki korogakoroga, kasha ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
|