Beijing ni mji mkuu wa China, katika mji huu kuna mabaki mengi ya kihistoria na kiutamaduni ukiwemo ukuta mkuu na kasri la kifalme, ambavyo ni maarufu sana duniani. Kwenye mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani, ambao uko kwenye sehemu ya kaskazini magharibi mwa China, umbali wa kilomita 1,000 hivi kutoka mji wa Beijing, kuna sehemu moja inayoitwa "Beijing ndogo iliyoko kwenye sehemu ya mpaka wa kaskazini mwa China".
Katika historia Bayinhaote iliyoko kwenye mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani inaitwa "Beijing ndogo iliyoko sehemu ya kaskazini". Katika lugha ya Kimongolia, Bayinhaote ni "mji wenye rasilimali nyingi", na ni mji ulioko upande wa magharibi kabisa kwenye mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani. Eneo la Alashan ni kubwa sana, lakini nusu yake ni jangwa, Bayinhaote ni sehemu moja yenye maji na mimea kwenye eneo hilo kubwa la jangwa. Ingawa tarafa hiyo si kubwa, lakini ni tarafa yenye jadi ya kizamani
Zaidi ya miaka 280 iliyopita, mtemi aliyekuwa kwenye mkoa wa Qinghai, kaskazini magharibi mwa China aliongoza wafuasi wake kufanya uasi, jamaa wa mfalme wa kabila la Wamongolia kwenye mkoa wa Mongolia ya ndani, aliamriwa kuongoza jeshi kwenda kutuliza uasi, na alitoa mchango mkubwa. Hivyo utawala wa wakati ule uliamua kumpa zawadi kwa kumjengea mji, ambao ni mji wa Bayinhaote wa sasa.
Baada ya ujenzi wa mji kukamilika, watu wa makabaila mengi wa wakati ule walihamia kwenye mji huo, mwaka nenda mwaka rudi, ukatokea ukoo mkubwa wa kifalme. Watu wa ukoo huo walifanya ujenzi, mtindo na ufahari wa majengo vinafuata na majengo ya makazi ya mfalme ya mjini Beijing. Nyumba nyingi za wakazi wa kawaida zilifanana na nyumba za wakazi wa mjini Beijing za wakati ule, ambazo zinajengwa kwenye pande nne na kuweka ua wa nyumba kwenye sehemu ya kati, kwa hiyo watu waliita Bayinhaote kuwa ni "Beijing ndogo iliyoko kaskazini mwa China". Mkurugenzi wa idara ya ujenzi wa mji wa Alashanzuoqi, ambao ipo tarafa ya Bayinhaote, Bw. Wang Jianping alisema,
"Kwa nini Bayinhaote inaitwa Beijing ndogo? Kwa sababu inasimamiwa moja kwa moja na serikali ya Beijing, tena, majengo na mji ulijengwa kwa kufuata mtindo wa Beijing."
Mpango wa ujenzi wa tarafa ya Bayinhaote ulifuata umbo la neno la Kichina "?", ambalo maana yake ni "bwana". Sehemu ya juu kabisa ni jumba la kaka wa mfalme, ina maana ya kuwa "kaka wa mfalme ni bwana wa huko"; kuna mifereji mitatu iliyopita mbele ya jumba la kaka wa mfalme kutoka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi, jinsi ilivyo ni kama mfereji uliopita kwenye sehemu ya mbele ya jumba la mfalme wa Beijing, mtu akitaka kuingia kwenye jumba la kaka wa mfalme, sharti apite kwenye mifereji hiyo mitatu. Mifereji hiyo mitatu ni kama mistari "?" katika neno la "?", maana ya "?" ni tatu, na barabara moja iliyotengenezwa kutoka lango la jumba la kaka wa mfalme ya kwenda upande wa kusini, ni kama mstari mmoja unaopita katikati kwenye neno la "?", huu pia ni umaalumu mkubwa wa "Beijing ndogo iliyoko kwenye sehemu ya kaskazini.
Inasemekana kuwa hapo zamani Bayinhaote ilikuwa na bustani yenye majengo yanayofanana na "Bustani ya majira ya joto" ya mfalme ya mjini Beijing. Sasa bustani hiyo imekuwa ni mahali pa kupumzika na burudani. Hapo mwanzoni katika bustani hiyo, kulikuwa na miti na maua mengi kama yaliyopo kwenye Bustani ya majira ya joto ya Beijing. Mbali na hayo, upande wa mashariki wa bustani hiyo ni kaburi la kaka wa mfalme, na upande wa magharibi kuna bustani inayoitwa bustani ya magharibi, upande wa kaskazini kuna jumba la kaka wa mfalme la kukwepa joto katika majira ya joto, ni kweli kuwa jumba zima la kaka wa mfalme linafanana kidogo na mji wa Beijing.
Ingawa Bayinhaote imekuwa na historia zaidi ya miaka 280, lakini iko kwenye jangwa, kwa hiyo hadi kabla ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China mwaka 1949, sehemu hiyo ilikuwa ni tarafa yenye eneo la kilomita za mraba elfu 30 hivi. Hapo zamani, sehemu ya Bayinhaote ilikuwa na maduka kadhaa karibu na jumba la kaka wa mfalme, lakini hivi sasa eneo la Bayinhaote limefikia kilomita za mraba elfu 80, ambapo kuna shule karibu 50, na idadi ya watu inakaribia laki 1.5. Barabara ile ya zamani iliyokuwa inaenda kwenye jumba la kaka wa mfalme, hivi sasa imebadilika kuwa barabara zinazoenda kila mahali, ambazo kuna magari na pikipiki nyingi zinazopita. Zana za mawasiliano ya habari zinazoiunganisha sehemu hiyo na sehemu mbalimbali za dunia, zinaifanya sehemu hiyo iungane na mambo ya kisasa.
Sehemu ile ya zamani lilipo jumba la kaka wa mfalme, sasa imebadilika kuwa sehemu ya mji wa zamani, katika sehemu hiyo kuna maduka na masoko mengi, hususan maduka yanayouza vito na mapambo ya crystal hujaa wateja. Hali ya sehemu mpya ni tofauti kabisa, barabara moja kubwa ya lami inapita katikati ya mji na kuelekea mbali kwenye mlima wa Helan, majumba marefu yamejengwa kwenye kando mbili za barabara hiyo. Kitu kinachovutia watu zaidi ni sanamu nyeupe ya ngamia mwenye nundu mbili iliyojengwa kwenye upande wa mashariki wa mji, sasa sanamu hiyo imekuwa nembo ya mji wa Bayinhote.
Huenda watu watauliza: kwenye sehemu ya jangwa, hali ya hewa ni ya ukame na yenye upepo mwingi, mbona Bayinhote ina miti na maua mengi, na ni kinyume cha hali ya hewa ya jangwani. Inaonekana kuwa sehemu hiyo imekuwa na hali ya hewa maalumu, na ilikuwaje kukawa na hali ya hewa ya namna hiyo? Mkurugenzi wa idara ya ujenzi wa mji, Bw. Wang Jianping alisema, hali hii inatokana na kazi ya uhifadhi wa mazingira, alisema,
"Watawala wa enzi mbalimbali walitilia maanani hifadhi ya mazingira ya Bayinhaote, walifanya usimamizi mkali kuhusu matumizi ya maji na ardhi, na kutoruhusu kujenga nyumba kiholela. Baada ya kuasisiwa kwa China mpya, serikali ya huko siku zote imekuwa inafuata utaratibu wa zamani katika ujenzi wa mji na upandaji wa miji na majani, kila mwaka inatenga fedha nyingi ili kuhakikisha ufanisi wa kazi hizo.
Idhaa ya kiswahili 2008-06-02
|