Tokea miaka ya 80 ya karne iliyopita, wafanyabiashara wengi kutoka Taiwan walikuja kuwekeza uwekezaji na kuanzisha shughuli zao China bara. Kutokana na maendeleo makubwa ya uchumi wa China bara, wafanyabiashara hao wamepata faida kubwa. Hivi sasa wafanyabiashara wengi zaidi kutoka Taiwan wamekuja kufanya biashara China bara, hata familia zao zimehamia China bara. Katika kipindi hiki cha nchi yetu mbioni, tutawaletea maelezo kuhusu Bw. Chen Fengrong ambaye amefanya biashara China bara kwa miaka 20.
Bw. Chen Fengrong ni meneja mkuu wa kampuni ya Quantong ya Taiwan, ambaye mababu zake walitoka mji wa Quanzhou mkoaji Fujian. Mwaka 1986 alifanya uchunguzi mjini Guangzhou. Wakati huo mji huo bado ulikuwa nyuma, lakini aliamua kuwekeza huko. Alijenga gati kwenye bandari ya Huangpu na kushughulikia uchukuzi wa bidhaa. Alisema alifanya uamuzi huo kwa sababu wakazi wa China bara na wa Taiwan wana utamaduni mmoja na wana uhusiano wa kindugu, na pia aliona kuwa uchumi wa China bara una uwezo mkubwa wa kupata maendeleo. Aidha, sera za kuwanufaisha wafanyabiashara wa Taiwan zinazolenga kuvutia uwekezaji wao ni sababu nyingine muhimu, iliyofanya aamue kuwekeza.
Bw. Chen alisema kutokana na tofauti ya sera na maoni kati ya China bara na Taiwan, mwanzoni alikabiliwa na matatizo mengi. Lakini kutokana na msaada wa serikali ya mji wa Guangzhou na idara husika, alitatua matatizo hayo, alisema,
"Nilipokuja kufanya biashara mjini Guangzhou, serikali ya mji huo ilinisaidia kushughulikia kazi mbalimbali. Nilipata uungaji mkono wa serikali katika pande mbalimbali. Sisi wafanyabiashara wa Taiwan tumenufaika na sera za upendeleo za serikali."
Kutokana na sababu hizo, shughuli za Bw. Chen Fengrong zilianza kupata maendeleo ya haraka. Yeye ni mtu mwenye moyo wa dahti na urafiki, hivyo wafanyakazi wanapenda kushirikiana naye. Mfanyakazi wa kampuni yake Bi. He Hongmei alisema,
"Tunakula chakula kwenye nyumba ya meneja mkuu wakati wa sikukuu. Yeye ni mtu mwenye moyo wa kirafiki, anawafuatilia wafanyakazi. Hapendi kuonesha kuwa yeye ni mkuu."
Maendeleo ya haraka ya uchumi wa China bara yamewavutia watu wengi zaidi kuja kufanya kazi hapa, ambayo yamesaidia maendeleo ya shughuli za Bw. Chen Fengrong. Naibu meneja mkuu anayeshughulikia biashara Bw. Qiu Shengjie pia anatoka Taiwan. Alijiunga na kampuni ya Quantong kwa sababu alitambua fursa nyingi za maendeleo ya uchumi wa Guangzhou na hata uchumi wa China bara, alisema,
"Nafirkiki kuna fursa nyingi za kibiashara mjini Guangzhou, uchumi wa mji huo mzuri, ambao ni karibu sawa na wa miji ya Taiwan. Maonesho ya bidhaa zinazouzwa na kuagizwa nje ya China yanafanyika kila mwaka, na pia kuna maonesho mengine mengi, kuna fursa nyingi. Hivyo nafiriki ni vizuri kuishi na kufanya kazi hapa."
Katika miaka 20 iliyopita, shughuli za Bw. Chen Fengrong zilipata maendeleo hatua kwa hatua. Licha ya shughuli kwenye gati, Bw. Chen alianzisha kampuni ya biashara mjini Guangzhou na kampuni ya kurudisha rasilimali mkoani Fujian. Hivi sasa pia anashughulikia kituo cha ufugaji wa samaki aina ya Tilapia. Amesaini mikataba na wakulima, kuwapatia wakulima samaki wadogo, wakulima wanafuga samaki, na ananunua samaki kutoka kwa wakulima hao.
Hivi sasa kituo hicho kinaweza kuzalisha samaki milioni 50 kwa mwaka. Bw. Chen ana matumaini makubwa kuhusu ufugaji wa samaki wa aina hiyo, alisema,
"Biashara ya samaki ya Tilapia mkoani Guangdong ni nzuri, na uuzaji wa samaki hao nje ni mkubwa, bado hauwezi kukidhi mahitaji soko. Hivyo tunaingiza samaki wadogo wazuri wa aina hiyo kutoka Taiwan na kuwafuga hapa."
Bw. Chen alieleza kuwa anapowauzia wakulima samaki wadogo, pia anawapatia wakulima ufundi wa kuwafuga samaki. Ana matumaini kuwa atashirikiana na vijiji kujenga kituo cha vielelezo ili kuwapatia wakulima ufundi zaidi.
Bw. Chen ameishi na kufanya kazi mjini Guangzhou kwa miaka 20, maendeleo na mabadiliko makubwa ya mji huo yamempatia kumbukumbu nyingi. Hivi sasa familia yake imehamia mjini humo. Amenunua nyumba na ana matumaini kuwa ataendelea kuishi mjini humo baada ya kustaafu, alisema,
"Mababu zetu walitoka China bara, vizazi 6 au 7 vimeishi huko Taiwan, na kurudi China bara ni matumaini yetu. Nimewaleta watoto wangu hapa, na wamesoma shule na chuo kikuu cha China bara. Watoto wote wataendelea kuishi hapa."
Alipozungumzia maendeleo ya uchumi wa China bara, alisema,
"Maendeleo ya miji mbalimbali ikiwemo Guangzhou, Shenzhen na shanghai ni makubwa sana. Hata katika miaka 10 hadi miaka 15 ijayo, Chna bara itaendelea kuwa na maendeleo. Tuna matumani makubwa kuhusu ongezeko la uchumi wa China bara, hivyo niliwaambia watoto wangu kuwa tutafanya shughuli zetu China bara. Nina matumaini kuwa watafanya kazi kwa makini, na hivi sasa wanafanya vizuri."
Maendeleo makubwa ya uchumi wa China bara yatawavutia wafanyabiashara wengi zaidi wa Taiwan kufanya kazi na kuishi China bara, na wataendeleza shughuli zao kutokana na mazingira mazuri ya maendeleo ya hapa.
|