Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-12 16:33:23    
Mwigizaji kijana wa mchezo wa opera ya kunqu Kunqu ya China Bw. Yu Jiulin

cri

Mchezo wa opera ya kunqu Kunqu ambayo hadi sasa imekuwa na historia ya miaka zaidi ya 600 inasifiwa kama ni chimbuko la aina zote za opera za jadi nchini China, ni sanaa iliyoorodheshwa na shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO katika urithi wa utamaduni usioonekana duniani. Bw. Yu Jiulin mwenye umri wa miaka 30 ni mwigizaji mashuhuri wa opera hiyo. Tangu mwaka 2003 Bw. Yu Jiulin alipoanza kujifunza namna ya kuigiza mchezo wa opera ya kunqu "Kibanda cha Peony" mpaka sasa ameonesha mchezo huo ndani na nje ya China kwa mara zaidi ya 140 na alipata tuzo ya heshima kubwa ya uigizaji wa opera za China.

Mchezo wa opera ya kunqu unaoitwa "Kibanda cha Peony" ilihaririwa kwa mujibu wa hadithi ya kale yenye jina hilo hilo ikieleza mapenzi ya kusikitisha kati ya mvulana Liu Mengmei na msichana Du Liniang. Msichana Du Liniang wa familia ya maofisa alikutana na msomi maskini Liu Mengmei katika bustani ya nyumbani kwa msichana Du Liniang na wakapendana, lakini kutokana na familia ya Du Liniang kutomwunga mkono, na kutokana hadhi tofauti ya kijamii kati yao, wapenzi hao wawili hawakuweza kuoana kama ilivyokuwa kwa Romeo na Juliet.

Yu Jiulin ni mwigizaji wa Kundi la Mchezo wa opera ya kunqu Kunqu la Suzhou mkoani Jiangsu. Miaka kadhaa iliyopita, alikuwa kama walivyoona wenginne kuwa sanaa ya opera hiyo haitakuwa na mustakbali mzuri. Wakati huo watazamaji wa opera hiyo walikuwa wachache sana, na hali ya kundi la mchezo wa opera ya kunqu Kunqu pia ilikuwa ya kusikitisha, michezo iliyokuwa inavutia sana imepoteza watazamaji. Hali hiyo iliwafanya waigizaji waoneshe vipande vya opera hiyo kwenye sehemu za utalii.

Mwaka 2002 msomi wa kisiwani Taiwan Bw. Bai Xianyong alikwenda kwenye Kundi la Mchezo wa opera ya Kunqu la Suzhou akiwa na matumaini ya kufufua sanaa hiyo na kuamua kuhariri mchezo wa opera ya kunqu unaoitwa "Kibanda cha Peony" akiwalenga vijana. Alishirikiana na wataalamu wengi kuhariri na kuchagua waigizaji. Bw. Yu Jiulin alichaguliwa kuwa mwigizaji mkubwa katika opera hiyo.

Ili aweze kuigiza vizuri mchezo wa opera ya kunqu wa "Kibanda cha Peony" alijifunza mengi kutoka kwa mwigizaji mzee Wang Shiyu. Hadi sasa Bw. Yu Jiulin anakumbuka jinsi alivyomwomba mzee huyo awe mwalimu wake. Alisema,

"Mzee Wang anaheshimiwa sana katika sanaa ya mchezo wa opera ya kunqu Kunqu. Mzee Wang alinipima toka utosini hadi kwenye nyayo kama alivyochagua mwigizaji, mwishowe alikubali kuwa mwalimu wangu. Furaha yangu ilikuwa haina kifani."

Kutokana na desturi, katika mambo ya sanaa mwanafunzi anapoomba fulani awe mwalimu wake ni lazima ampigie magoti. Ingawa Yu Jiulin hakumpigia magoti mzee Wang, mzee huyo alikuwa anamfundisha kwa makini sana toka namna ya kuimba mpaka namna ya kufanya vitendo ili kuonesha hisia za ndani za mhusika wa hadithi hiyo ya "Kibanda cha Peony". Kutokana na kuwa wakati huo Yu Jiulin alikuwa na miaka zaidi ya 20, ilikuwa ni vigumu kwake kufanya vitendo vingi kama alivyotakiwa kutokana na kukomaa, mazoezi yalikuwa magumu sana. Alisema,

"Mazoezi ya viungo yalikuwa magumu sana ingawa nilipokuwa katika shule ya opera nilifundishwa, lakini kutokana na kuwa na umri mkubwa mazoezi yalikuwa magumu kweli."

Bw. Yu Jiulin alisema, mazoezi hayo yalimsaidia sana kuonesha vizuri mchezo wa opera ya kunqu unaoitwa "Kibanda cha Peony", alisema Bwla mazoezi hayo ya mchezo wa opera ya kunqu usingeweza kuoneshwa vizuri kama sasa na kuwavutia sana watazamaji vijana. Jambo ambalo linamfanya kumheshimu sana mzee Wang ni kwamba kila mara alipoonesha mchezo huo mwalimu Wang alikuwa anakaa kwenye nafasi ya watazamaji na kumhimiza aoneshe vizuri zaidi.

Mwezi Aprili mwaka 2004 kwa mara ya kwanza mchezo huo ulioneshwa katika kisiwa cha Taiwan. Matangazo ya mchezo huo yalibandikwa kwenye kila kituo cha subway. Bw. Yu Jiulin alikumbuka kwamba watazamaji walikuwa wanajaa ukumBwni na kulipokuwa na ukimya wakati mchezo uliopooneshwa, hata sauti ya kudondoka kwa sindano inasikika, na jinsi watazamaji walivyovutia pia ilionekana katika maonesho ya baadaye zaidi ya mara mia moja. Mwaka 2006 mchezo huo ulioneshwa mara nne nchini Marekani, watazamaji waliufurahia sana. Yu Jiulin alisema,

"Karibu kila baada ya maonesho kumalizika ilituBwdi kurudi tena jukwaani kutoa shukurani kwa dakika 15 hivi kutokana na makofi ya muda mrefu. Kutokana na kuwa kabla ya hapo michezo ya opera za China iliyooneshwa katika nchi za nje mingi ilikuwa ni michezo iliyoonesha gongfu na hawakuwahi kuona mchezo wa opera ya kueleza mapenzi kama mchezo huo wa "Kibanda cha Peony", walishangaa kumbe sanaa ya jadi ya China ni nzuri sana."

Sasa licha ya mchezo wa "Kibanda cha Peony" kuhaririwa kuwa mchezo wa opera ya Kunqu pia umehaririwa kuwa dansi ya ballet. Bw. Yu Jiulin alisema hakutegemea kama mchezo wa mchezo wa opera ya kunqu Kunqu ungewafanya tena Wachina waupende utamaduni wao wa jadi. Alisema,

"Mchezo wa mchezo wa opera ya kunqu wa 'Kibanda cha Peony' umeleta taathira kubwa ya kijamii, ingawa baadaye maonesho ya mchezo huo hakika yatapungua, lakini kutokana na mchezo huo watazamaji wameanza kufuatilia sanaa ya opera za jadi. Tutaendelea kuhariri michezo mipya ya opera ya kunqu, na hamu ya watazamaji kuangalia mchezo wa opera ya kunqu jadi haitapungua."

Bw. Yu Jiulin alisema, mwezi Juni baada ya kuonesha mchezo huo nchini Uingereza wataanza kufanya mazoezi ya maigizo ya mchezo mwingine uitwao "Kibanio cha Jadi cha Nywele". Huu pia ni mchezo wa opera ya kunqu unaoeleza mapenzi kati ya mvulana na msichana.

Idhaa ya kiswahili 2008-6-12