Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-25 17:55:03    
Wanafunzi wanaotoka nje wa shule ya msingi ya Zhongying ya mji wa Shenzhen waishi kwa furaha kwenye mbuga

cri

Tukizungumzia mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani ulioko kaskazini mwa China, watu hukumbuka mbuga kubwa ya majani, chai ya maziwa na wafugaji wakarimu wa kabila ya wamongolia, pamoja na mila na desturi za kimongolia zenye historia ya miaka elfu moja. Hivi karibuni wanafunzi 86 wanaotoka nje wanaosoma mjini Shenzhen walikwenda kwenye shule moja ya msingi ya mkoa unojiendesha wa Mongolia ya ndani kushiriki kwenye shughuli za maingiliano ya kielimu. Katika wiki hizo mbili, wanafunzi hao walijionea wenyewe maisha na utamaduni wa watu wa kabila la waMongolia.

Wanafunzi hao 86 wote wanasoma darasa la tano katika shule ye msingi ya Zhongying ya mji wa Shenzhen, kwa kuwa wanafunzi hao wanatoka sehemu za Hongkong na Taiwan, na nchi za Korea ya Kusini, Japan na Philippine, kwa hiyo wao kweli ni "wanafunzi wadogo kutoka nje", na shule ya msingi ya No. 2 ya majaribio ya kiwanda cha chuma na chuma cha pua cha Baotou ilipewa jukumu la kuwapokea wanafunzi hao.

Katika shule hiyo wanafunzi hao wadogo walichanganywa katika madarasa mbalimbali na kufundishwa kwa zamu na walimu wa shule hizo mbili, wanafunzi hao walijifunza kwa pamoja na kubadilishana uzoefu wa masomo. Mkuu wa shule hiyo ya Baotou Bw. Dai Yunhai alipozungumzia ushirikiano huo alisema:

"kwa kuwa tuko kwenye sehemu ya ndani ya China, tumeona kuwa kweli kutokana na ziara hiyo ya walimu wa Shenzhen, tuna mambo mengi ya kujifunza, hasa katika mtizamo wa ufundishaji. Tumeingiza njia hiyo mpya ya mawasiliano ya elimu, na kuweka utaratibu mzuri kwa walimu na wanafunzi, katika siku za baadaye, shughuli nyingi zaidi zenye manufaa zitafanyika kwa kupitia utaratibu huo."

Kwa watoto wa shule ya msingi ya Zhongying, mbali na kujifunza pamoja darasani, mawasiliano nje ya darasa na kutembelea familia za wamongolia pia zilikuwa ni sehemu muhimu za maisha yao kwenye mbuga. Mwanafuzi The Hui Tuyaa anatoka famlia ya waMongolia, ingawa anaishi kwenye mji wa kisasa, lakini familia yake bado inaendelea kufuata desturi nyingi za kimongolia, kwa mfano wanazungumza kwa kimongolia, wanakunywa chai ya maziwa, wanaimba nyimbo za jadi na kuwatukuza mshujaa wa kabila la waMongolia katika historia Ghinggis Khan. Wanafunzi wadogo kutoka nchi za Korea ya Kusini, Japan na Philippines walioalikwa kutembelea familia hiyo walifanya urafiki haraka na familia hiyo.

Baba wa The Hui Tuyaa aliwasimulia watoto hao hadithi za Ghinggis Khan, na kuwafahamisha zaidi kuhusu historia ya ajabu ya kabla ya Wamongolia iitwayo "kabila la kwenye mgongo wa farasi". Wanafunzi hao wengi wana hamu ya kujifunza lugha ya Kimongolia, mama ya The Hui Tuyaa aliwafundisha kuwa "Saibainu" maana yake ni "Karibu", watoto walifurahi sana na hata kusalimia kila mtu waliyemwona kwa "Saibainu".

Kutembelea familia ya The Hui Tuyaa waliweza kujua ukarimu na upole wa watu wa kabila la wamongolia, hata walirudia mara kwa mara kusema kwa kichina "nafurahi sana." Kufanya urafiki na watoto hao wa nje pia kulimfurahisha sana The Hui Tuyaa. Alisema:

"naona watoto hao ni wapole sana. Niliwapokea kwa ukarimu kwa chai ya maziwa na kuwapa hada, na niliwapa zawadi maalum za Mongolia ya ndani, ni matumaini yangu kuwa wataweza kukumbuka kwamba watu wa waMongolia ni wachangamfu na wakarimu sana."

Baada ya masomo, wanafunzi hao wadogo walipanda farasi na ngamia, walipiga mishale na kusikiliza nyimbo za kimongolia, wakajionea mandhari ya mbuga na mila na desturi za kimongolia; kwenye uwanda wa juu wa Erdos, watoto walijaribu kuteleza juu ya michanga; kwenye jumba la maonesho ya kampuni ya chuma cha pua cha Baotuo ambayo ni kituo muhimu cha kuzalisha chuma na chuma cha pua nchini China, watoto hao walifahamishwa kuhusu historia ya maendeleo ya mji wa Baotou, walishangaa sana walipofahamu kuwa mji huo mzuri wa kisasa ulijengwa miaka 50 iliyopita kwenye jangwa. msichana kutoka Korea ya Kusini Baek Seng Heen mwenye umri wa miaka 11 alipozungumzia jinsi alivyouona mkoa wa Mongolia ya ndani alisema:

"naona nyimbo na ngoma za kimongolia zinavutia sana, pia nimefahamu kiasi mila na desturi za kabila la wamongolia. Wamongolia ni watu wakarimu sana, nilifanya urafiki nao, ambayo ni kumbukumbu yangu ambayo sitasahau kuhusu mji huo!"

Kuishi kwa pamoja kwa siku chache tu kumewafanya watoto kutoka sehemu mbili wapatane na kuwa na urafiki mkubwa. Watoto wa mji wa Baotou waliwasifu sana watoto kutoka nje kwa uwezo wao wa kujihudumia katika mambo ya maisha, ushupavu wa kujibu maswali darasani na mawazo yenye uchangamfu; watoto kutoka nje pia wamekuwa na maoni yao. Mtoto Baek Seng Heen kutoka Korea ya Kusini alisema, kwa kuwa hawezi kuzungumza vizuri kichina, pia hapendi kuongea sana, alikuwa na wasiwasi wa kuwa na upweke kwenye mazingira mapya, lakini ukarimu na urafiki wa watoto wa Baotou uliondoa kabisa wasiwasi wake. Baek Seng Heen alisema:

"nadhani sikuwa na sababu ya kuwa na wasiwasi, wanafunzi hao ni wakarimu sana, naona furaha sana kuishi pamoja nao."

Shughuli hiyo iliwafahamisha wazi walimu na wanafunzi wa shule hizo mbili kuhusu tofauti na umaalum wa utamaduni na elimu za sehemu mbili, pia ilitoa fursa kwao kufundishana. Mkuu wa shule ya msingi ya Zhongying ya Shenzhen Bw. Guo Donggan alisema:

"shughuli hiyo ya maingiliano kati ya shule zetu mbili, watoto walikuja kujionea hali ya hewa, mazingira ya kiutamaduni na mazingira ya kujifunza, nadhani hii itasaidia ukuaji wao."