Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-07-02 20:10:39    
Mtaalamu kutoka Uholanzi anayefanya kazi katika taasisi ya uhandisi wa magari ya China Bw. J. Post

cri

Katika miaka ya hivi karibuni, hewa chafu zinazotolewa na magari yanayoongezeka siku hadi siku zimekuwa tishio kubwa kwa mazingira, utafiti kuhusu magari yanayotumia gesi ambayo hayatoi uchafuzi na yanayobana matumizi ya nishati umekuwa eneo la sayansi na tekonolojia linalofuatiliwa kote duniani. Taasisi ya uhandisi ya magari ya China iliyoko kusini magharibi mwa mji wa Chongqing ni kituo cha kwanza cha utafiti kuhusu teknolojia za uhandisi wa magari yanayotumia gesi nchini China, kwa miaka mingi iliyopita, kituo hicho kimendelea kujitahidi katika eneo hilo. Bw. J. Post ni mtafiti mwandamizi wa taasisi hiyo, ingawa ana umri wa miaka 33 tu, lakini amepewa "tuzo la urafiki la taifa la China" ambalo ni tuzo la kiwango cha juu kabisa linalokabidhiwa na serikali ya China kwa wataalamu kutoka nchi za nje kutokana na michango yao kwa China.

Kwenye ofisi ya Bw. Post, vipuri vya gari vilikuwa vinaonekana kila mahali. Masanduku mawili ya mizigo yalikuwa kandoni mwa meza yake, kwa kuwa alirudi hivi karibuni kutoka Iran, na alisema amezoea kusafiri pamoja na vifaa vingi kama hivyo kwenye sehemu mbalimbali kote duniani.

Bw. Post amefanya kazi kwenye taasisi ya uhandisi wa magari ya China kwa miaka mitatu, mwaka 2003 Bw. Post alikuwa maneja wa taasisi ya utafiti wa magari katika Shirika la utafiti wa sayansi ya matumizi la Uholanzi, na kwa niaba ya kampuni yake alianzisha ushirikiano wa utafiti kuhusu magari yanayotumia gesi na kampuni ya Chang'an ya Chongqing na taasisi ya uhandisi wa magari ya China. Katika muda wa ushirikiano huo, Bw. Post alisifiwa na wenzake wa China kwa uzoefu na uwezo wake. mwezi Mei mwaka 2005, alipewa mwaliko wa ajira na taasisi ya uhandisi wa magari ya China, kwa hiyo alijiuzulu kazi yake na kuuza nyumba yake nchini Uhonlanzi, na alikwenda Chongqing.

"naipenda China, tumeshirikiana vizuri sana. Kufanya uamuzi wa kubaki nchini China kweli ni changamoto mpya."

Kwenye mazingira mazuri yanayoheshimu ujuzi, wataalamu na kuhamasisha uvumbuzi, Bw. Post ametoa mchango mkubwa kwenye eneo la utafiti wa magari yanayotumia gesi, na alishiriki kwenye usanifu wa teknolojia za magari yanayotumia gesi na ijini yake, na teknolojia hizo zimeziba pengo kwenye eneo hilo nchini China. Kutokana na michango yake mikubwa, mwaka 2005 alipewa tuzo ya urafiki wa magenge matatu ya mji wa Chongqing, mwaka 2006 alimekuwa mtu mwenye umri mdogo kabisa aliyepewa tuzo ya urafiki wa taifa wa China.

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi na jamii ya China, idadi ya magari imeendelea kuongezeka, na matatizo mengine pia yameanza kutokea yakiwemo utoaji wa hewa chafu za magari na matumizi ovyo ya nishati, hali hiyo imehimiza serikali ya China kutilia maanani utafiti wa magari yanayotumia gesi. Bw. Post alisema alishuhudia mafanikio yaliyopatikana nchini China katika eneo hilo. Bw. Post alisema:

"magari yanayotumia gesi yanatumia nishati safi, yanaweza kupunguza hali ya uchafuzi wa hewa unaotokana na utoaji wa hewa chafu za magari mengi kwenye miji mikubwa. Katika miaka ya hivi karibuni utafiti wa eneo hilo umepata maendeleo makubwa nchini China, katika miaka kadhaa iliyopita, tulipata maendeleo kutoka kutumia gesoline ya kawaida hadi dizeli na hadi kutumia gesi iliyoshinikizwa ya hivi sasa. Teknolojia yetu ya mfumo wa kuingiza gesi imefikia kiwango cha kimataifa. Kwa kwaida, inachukua muda wa miaka 10 hadi 15 kufikia kiwango hicho, lakini tulitumia miaka 2 hadi 3 tu. Utafiti huo kweli umepata maendeleo makubwa nchini China."

Bw. Post alipozungumzia hali ya kuenea kwa magari yanayotumia gesi nchini China, alisema licha ya texi na mabasi yanayotumika katika mkoa wa mkoani Sichuan mwenye raslimali nyingi za gesi za kimaumbele, hivi sasa magari yanayotumia gesi bado hayajatumiwa sana nchin China. Bw. Post alisema, serikali ya China imetambua mustakabali mkubwa wa magari ya aina hiyo katika kuhifadhi mazingira na nishati, ikiimarisha ujenzi wa miundombinu husika, magari ya aina hiyo yataenea kwa haraka nchini China.

kwenye njia ya kuelekea maabara, mwandishi wetu wa habari aliona magari ya aina mbalimbali kwenye uwanja, Bw. Post alieleza kuwa magari yote hayo yanatumia gesi, akipointi katika gari moja la mizigo lenye rangi ya machungwa alisema:

"hili ni gari jipya tulilolisanifu na linaloweza kutumia nishati za aina tatu, yaani gesoline, gesi ya kimaumbile na alcohol, na hata linaweza kutumia nishati mchanganiko kwa kiasi chochote wa gesoline na alcohol."

Bw. Post aliendelea kueleza kuhusu idara mbalimbali za utafiti kama vile maabara, kituo cha upimaji wa ubora na maabara ya magari mazima. Mbele ya maabara ya upimaji wa utoaji wa hewa chafu, Bw. Post alisimama na alisema:

"maabara hayo ni idara inayopima utoaji wa hewa chafu za magari, pia ni sehemu tunapofanya kazi kwa muda mrefu kabisa."

Mafanikio yaliyopatikana Bw. Post hayaondokana na bidii na juhudi zake. Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa mgari yanayotumia gesi Bw. Li Jingbo alisifu sana uwezo wa kazi wa Bw. Post, alisema:

"Hii ni mara ya kwanza kwangu kona mtaalamu kutoka nje mwenye bidii kama yeye. Mbali na uwezo wake mkubwa kuhusu teknolojia, kama ikihitajika, hata anaweza kukwenda chini ya gari, anaweza kufanya kazi nyingi ambazo sisi wachina hatufikiri wataalamu kutoka nje watazifanya. Aidha, Bw. Post ni mtu mkamili, si kama tu katika teknolojia, bali pia katika biashara, katika kushughulikia mahusiano na nje, hasa kwamba kwa kupitia yeye tumekuwa na mawasiliano mengi zaidi na makampuni ya nje. Yeye ni kama daraja kwetu la kwenda dunia ya nje."