Naibu mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya kuendeleza mashamba ya China Bw. Han Xiangshan, hivi karibuni alisema makampuni ya China yanatakiwa kuwekeza kwa wingi zaidi kwenye shughuli za kilimo barani Afrika, na kuanzisha mashamba makubwa yenye uzalishaji wa kiwango cha juu.
Bw. Han Xiangshan alisema Afrika ni sehemu inayofaa kuendeleza kilimo, na pia inahitaji kuendeleza kilimo. Ufundi wa jadi wa kilimo wa China unafaa sana hali ya maendeleo ya kilimo barani Afrika, kiasi cha faida baada ya uwekezaji kwenye kilimo barani Afrika ni kikubwa zaidi kuliko kile nchini China. Kwa mfano, nchini Zambia kiwango kati ya uwekezaji na upatikanaji wa faida kwenye mashamba ni kati ya asilimia 20 na asilimia 30. Bw. Han aliona kuwa kama mashamba hayo yanayowekezwa na China yanatakiwa kuimarishwa, ni lazima kuyafanya yawe makubwa zaidi na yanayozalisha mazao kwa kufuata utaratibu kamili.
Kuanzia mwishoni mwa mwaka 1993 alipokuwa ofisa wa kampuni hiyo hadi mwaka 2005 alipostaafu, Bw. Han Xiangshan alishughulikia miradi ya kuendeleza kilimo barani Afrika. Baada ya kustaafu alikwenda Zambia kuwekeza kwneye shughuli za kilimo. Mwezi Februari mwaka 2007, Shamba la Huafeng lililoanzishwa na Bw. Han Xiangshan pamoja na watu wengine lilizinduliwa. Hivi sasa shamba hilo lililowekezwa dola za kimarekani milioni 1.2 limekuwa shamba lenye ujenzi kamili.
Shamba la Zhongken la Zambia liko umbali wa kilomita mia kadhaa na Shamba la Huafeng pia linatekeleza kanuni ya maendeleo sawa na Shamba la Huafeng. Mkuu wa Shamba la Zhongken Bibi Li Li alimwambia mwandishi wa habari kuwa mpango wao kuhusu kupata mafanikio ni kwamba, wanapaswa kupanua shamba lao na kuliendeleza kwa utaratibu kamili.
Shamba la Zhongken lilianzishwa mwaka 1994, sasa lina eneo la hekta 4100. Hivi sasa kazi kuu ya shamba hilo ni ufugaji wa mifugo na kazi yake ya pili ni upandaji wa mimea. sasa limeendelezwa kuwa shamba kubwa ambalo mali zake zimekuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 5.43 na mapato kwa mwaka ni zaidi ya dola za kimarekani milioni 3.
Uzalishaji wa ngano kwa kila mwaka kwenye mashamba hayo ni tani 6 kwa kila hekta, kama bei ya ngano kwa kila tani ni dola za kimarekani 500, mapato ya uuzaji wa ngano yatafikia zaidi ya dola za kimarekani elfu 3 kwa kila hekta. Ikilinganishwa na uwekezaji wa moja kwa moja kwenye mashamba hayo ambayo ni chini ya dola za kimarekani 1300 kwa kila hekta, kiasi cha faida ni kikubwa sana baada ya kukata gharam na ushuru mbalimbali. Wakati huo huo, kutokana na gharama za matumizi ya ardhi na vifaa vya kilimo hazitabadilika sana, hivyo kama mashamba hayo yataendelezwa kuwa makubwa zaidi yataleta faida kubwa zaidi.
Bibi Li Li alisema, uendeshaji wa kazi ya ufugaji pia hauwezi kutengana na kanuni za kuendelezwa kuwa kazi kubwa zaidi na kufuata utaratibu kamili zaidi. Mwaka 2002,tawi la kiwanda cha ufugaji wa kuku cha Shamba la Chongken lilizinduliwa rasmi, zana na vifaa vya kisasa vya ufugaji wa kuku kwenye tawi hilo la kiwanda, vinasaidia tawi hilo kuongeza zaidi uzalishaji wa mayai. Mwaka 2007, Shamba la Zhongken lilikuwa na kuku laki 1.1 ambao walitaga mayai milioni 2.15, uuzaji wa mayai umechukua asilimia 10 kwenye soko la nchini Zambia.
Lakini Bibi Li Li alisema ikilinganishwa na mashamba makubwa yanayoendeshwa na watu wa magharibi, shamba la Zhongken bado lina nguvu ndogo. Ana matumaini ya kuongeza zaidi uwekezaji, ili kushindana na mashamba mengine makubwa.
Habari nyingine zinasema wataalamu wa kilimo wa China wananaofanya ushirikiano wa tekenolojia wa kupanda mpunga kwenye sehemu ya Podor nchini Senegal, waliwafundisha wakulima wa huko ufundi wa kilimo cha mpunga kutokana na hali halisi ya huko. Katika nusu mwaka uliopita, wamewafundisha wakulima zaidi ya 500 na kupata mafanikio makubwa.
Mku wa kikkundi cha wataalamu wa China Bw. Zheng Zheng alisema, wataalamu wa China walikwenda vijiji vya huko na kuwafundisha wakulima wa Senegal namna ya kupanda mpunga, kuwaongoza kutembelea mashamba ya vielelezo, kuwafundisha papo hapo na kutoa mafunzo kwenye darasa.
Kuenea ufundi wa kupanda mpunga unaoweza kupata mavuno makubwa, na kufanya mawasiliano ya ufundi wa mpunga ni kiini cha ushirikiano wa tekenolojia ya kilimo kati ya China na Senegal. Wataalamu wa mpunga kutoka kampuni ya kimataifa ya Yichang ya China walitoa maoni yao kuhusu uzalishaji wa mpunga kwenye sehemu karibu na Mto Senegal kwenye msingi wa uchunguzi na kutoa mpango wa tekenolojia na mafundisho.
Eneo la Podor liko kwenye Mto wa Senegal ambapo ni sehemu nzuri wa umwagiliaji, na kuna ardhi ya eneo lenye mita milioni 2.4 za mraba, lakini hivi sasa ardhi ya eneo hilo linalolimwa ni mita za mraba milioni 0.5. Kama ardhi hiyo ikitumiwa ipasavyo, Senegal itaweza kujitosheleza kwa mpunga.
|