
Tarehe 16 kwenye mchezo wa kuogelea mita 100 kwa mtindo wa kipepeo, mchezaji wa Marekani Phelps Michael amepata medali ya dhahabu, hii ni medali yake ya saba ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing.
Mchezaji wa Serbia Cavic Milorad amepata medali ya fedha kwenye mchezo huo, na mchezaji wa Australia Lauterstein Andrew amepata medali ya shaba.
Bw. Fhelps alipata medali 6 za dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Athens mwaka 2004, mpaka sasa amekuwa mchezaji aliyepata medali nyingi zaidi za dhahabu kwenye historia ya Michezo ya Olimpiki.

|