Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-01 17:11:04    
Mpango wa elimu ya michezo ya Olimpiki ya Beijing wafanya vijana wa China wajionee wenyewe michezo ya Olimpiki

cri

Michezo ya Olimpiki ya Beijing ina shughuli moja yenye uvumbuzi inayoonesha mtizamo wa "Olimpiki ya kiutamduni", shughuli hiyo inaitwa "mpango wa uelimishaji wa michezo ya Olimpiki ya Beijing". Kwa mujibu wa mpango huo, kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing itaweka asilimia 14 ya tiketi za michezo hiyo na kuwapatia fursa vijana wa sehemu mbalimbali nchini China waweze kuja kwenye viwanja na majumbe ya michezo hapa Beijing na kujionea wenyewe mvuto wa michezo ya Olimpiki.

Tarehe 19 Agosti, mashindano ya mchezo wa judo yaliendelea kufanyika kwenye jumba la michezo la chuo kikuu cha kilimo cha China. miongoni wa watazamaji, kulikuwa na mwanafunzi mmoja kutoka shule ya sekondari ya juu ya mji wa Lishui mkoani Zhejiang, jina lake ni Fang Dongshuo. Alisema anabahatika sana kupata fursa ya kutazama mashindano ya michezo ya Olimpiki papo hapo. Alifurahi sana, akisema:

"naona kweli nimebahatika sana kupata fursa hii kuja Beijing kutazama michezo ya Olimpiki. mimi nikiwa ni mwanafunzi, nafuatilia sana michezo, lakini zamani nilitazama mashindano kwenye televisheni, ingawa mashindano yenyewe ni mazuri sana lakini siwezi kujionea mwenyewe, safari hii nimekuja Beijing, nafurahi sana hata nashindawa kueleza maneno."

Tarehe 13 mwezi Julai mwaka 2001 wakati mji wa Beijing iliposhinda kuwa mwenyeji wa michezo ya 29 ya Olimpiki, Beijing iliahidi kufanya shughuli mbalimbali za uelimishaji za michezo hiyo ili kueneza moyo wa Olimpii kwa vijana milioni 400 wa China. kuanzia wakati huo, mpango wa uelimishaji wa michezo ya Olimpiki umeanza kutekelezwa, vijana milioni 400 wa China wakaanza kuikumbatia michezo hiyo kwa shauku. Kijana Fang Dongshuo pamoja na wenzake wakiwa ni kati ya vijana walionufaika na mpango huo walikuja Beijing kutazama michezo ya Olimpiki kama ilivyokuwa kwenye ndoto yao. Mwalimu aliyewaongoza katika safari hii Bw. Lu Xiaoxiao alisema:

"safari hii tumekuja walimu watatu pamoja na wanafunzi 7, hali tunavyoionea hapo papo kwenye kiwanja cha michezo ni tofauti kabisa na ile ilivyokuwa mbele ya televisheni. Tulitazamza mashindano ya mieleka, baseball na riadha, tumefahamu zaidi kuhusu michezo hiyo na ujuzi wa Olimpiki."

Kwa mujibu wa mpango uliowekwa na kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing, tiketi zipatazo milioni moja kwa ajili ya mpango huo zinachukua asilimia 14 ya tiketi zote za michezo ya Olimpiki zinazouzwa kwa nje, bei ya tiketi za mashindano ya mwanzo ni yuan 5, za fainali ni yuan 10, maana yake ni kuwamba mamilioni ya vijana wa China walipewa tiketi za michezo hiyo kwa bei ya chini kabisa. Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shule ya sekondari ya No. 2 ya Qingyuan ya mji wa Lishui mkoani Zhejiang Huang Ziwei alisema, ndiyo kutokana na michezo hiyo ya Olimpiki, alikuwa na likizo lisilosahaulika katika maisha yake. Alisema:

"nadhani kuwa nilipita likizo hili kwa furaha sana, kwa kuwa nimekuja Beijing kwa fahari kubwa kutamaza michezo ya Olimpiki, wakati wachezaji wa China wakiingia kwenye uwanja wa michezo, tunaona fahari kwao na tutawapigia makofi."

Mpango wa uelimishaji wa michezo ya Olimpiki ni ahadi ya makini iliyoshikiliwa kwa miaka 7, kabla ya kuanza kwa mashindano ya michezo hiyo, vitabu vya maelezo kuhusu michezo ya Olimpiki vimesambazwa darasani mwa shule za msingi na za sekondari, moyo wa Olimpiki pia umeweka mizizi mioyoni mwa vijana wa China. Fang Dongshuo alisema, alijifunza mambo mengi kutoka kwenye vitabu vya maelezo kuhusu Olimpiki, amepata mengi zaidi baada ya kuingia mwenyewe kwenye viwanja vya michezo ya Olimpiki.