Kwa msichana wa Zambia Lubas Shaqiba mwenye umri wa miaka 18, mwaka 2008 ni mwaka wenye maana maalumu. Katika miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2008, atasomea kozi ya uchumi hapa Beijing, msichana huyo kutoka Zambia amehusiana kwa karibu na China ambayo iko mbali na bara la Afrika.
Bi. Shaqiba alisema, katika miaka ya karibuni iliyopita, kasi ya maendeleo ya uchumi wa China inawashangaza watu, na uzoefu wa China unastahili kuigwa. Aliona kuwa kusomea kozi ya uchumi nchini China ni chaguo zuri.
Bi. Shaqiba ni mmoja kati ya wanafunzi waliopewa udhamini wa masomo nchini China mwaka 2008. Mwaka huu wanafunzi 46 kutoka Zambia walipewa udhamini huo. Huu ndio mwaka ambapo China ilitoa udhamini wa masomo kwa idadi kubwa zaidi ya wanafunzi wa Zambia.
Kwneye sherehe iliyofanyika hivi karibuni kwa ajili ya kuwaaga wanafunzi wa Zambia wanaopewa udhamini wa masomo nchini China, balozi wa China nchini Zambia Bw. Li Qiangmin alisema, maendeleo hayatapatikana bila elimu, na serikali ya China inapenda kuendelea kuisadia Zambia kuandaa watu wengi zaidi wenye ujuzi.
Takwimu husika zinaonesha kuwa, tangu mwaka 1978 China ilitoa udhamini wa masomo kwa idadi ya wanafunzi 500 wa Zambia wanaosoma nchini China. Hivi sasa serika ya China si kama tu imesamehe ada zao za masomo, malazi na matibabu, bali pia inatoa ruzuku ya maisha ya yuan 1,400 hadi 2,000 kwa kila mtu kwa mwezi.
Kwa niaba ya serikali ya Zambia, naibu waziri wa elimu wa Zambia Bw. Clemente aliishukuru serikali ya China kwa misaada ya elimu kwa Zambia katika miaka ishirini iliyopita. Bw. Clemente alisema wanafunzi wa Zambia waliosoma nchini China si kama tu wamekuwa nguvu kubwa ya maendeleo ya Zambia, bali pia walijenga daraja la urafiki kati ya nchi za China na Zambia zinazo mbali sana.
Meneja anayeshughulikia mawasiliano na nje wa benki ya Chartered nchini Zambia Bi. Shawa Manbuwe ni mwanafunzi hodari kati ya wanafunzi wa Zambia waliopewa udhamini wa masomo nchini China.
Mwaka 2001 Bi. Manbuwe alipokea taarifa ya kusoma kwenye Chuo kikuu cha uwalimu cha Huadong cha China. lakini mbele ya fursa hiyo ya masomo nchini China, Bi. Manbuwe alisitasita. Alisema alifikiri kwa muda mrefu, kwani anatakiwa kuwa na ushujaa mkubwa kuwaaga mume wake na watoto wake na kusoma peke yake nchini China.
Lakini hatimaye Bi. Manbuwe aliamua kuja China. alisema anafurahi sana kufanya uamuzi sahihi wakati ule, kwani kusoma nchini China kumeleta fursa nyingi zaidi kwa maisha yake.
Wateja wengi wa Senegal wanapenda bidhaa zilizotengenezwa na China
Kutokana na habari zilizotolewa hivi karibuni na gezeti la l' aurora nchini Senegal, matokeo ya uchunguzi wa soko uliofanywa na gazeti hilo yanaonesha kuwa Wateja wengi nchini Senegal wanapenda bidhaa zilizotengenezwa na China, na wanaona kuwa sifa za nguo, viatu na bidhaa nyingine za maisha zinazidi kuwa nzuri.
Habari hizo zinasema Wateja wengi wanaridhika na sifa za bidhaa zilizotengenezwa na China. Kwenye "mtaa mkubwa wa miaka mia moja" mjini Dakar ambapo kuna maduka mengi ya China, wakazi wa huko wanaonunua bidhaa za China wanaonekana ni wengi kutoka asubuhi hadi usiku. Kati yao kuna wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa za China, pia kuna Wateja binafsi.
Mfanyabiashra Bw. Saike alisema, alinunua jozi 12 za viatu vya kike kwenye maduka ya China kwa dola za kimarekani 4 kwa jozi moja, bei hiyo ni ya chini zaidi kuliko bei za viatu kwenye sehemu nyingine, aidha sifa za viatu ni nzuri sana, na vinapendwa sana na wanawake wa Senegal. Mfanyabiashara Bw. Mustafa alisema hivi sasa wasichana wengi wa Senegal wanapendelea kununua nguo za aina mpya zilizotengenezwa na China.
Nchini Senegal kila familia huwa na watoto wengi, tangu bidhaa zilizotengenezwa na China zilipoingia kwenye nchi hiyo, familia nyingi zenye mapato ya chini zimeona kuwa shinikizo lao linapungua. Wanaweza kuwanunulia watoto wao nguo nyingi kwa pesa chache. Bw. Aduma alinunua jozi 10 za soksi kwenye dula la China, alisema tangu bidhaa zenye sifa nzuri na bei nafuu zilizotengenezwa na China ziingie nchini Senegal, havai tena soksi mbovu.
|