Michezo ya Olimpiki ya Beijing imemalizika kwa mafanikio. Wachezaji zaidi ya elfu 10, waandishi wa habari zaidi ya elfu 30 na watazamaji na watalii zaidi ya laki moja wote wamejisikia furaha, fahari na ndoto zilizoletewa na michezo ya Olimpiki ya Beijing. Huduma za matibabu zikiwa ni hatua moja muhimu ya uhakikisho wa uendeshaji wa mashindano, madaktari wa Beijing pia wamefanya juhudi kuhakikisha matibabu kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing na michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Beijing.
Alasiri ya tarehe 19 Agosti, mashindano mbalimbali ya michezo ya Olimpiki ya Beijing yalipokuwa yanaendelea motomoto, kwenye chumba cha mapumziko cha timu ya mbio za baiskeli ya Afrika Kusini kocha wa timu hiyo Bw. Leon Schepers alishindwa kupumua na mapigo ya moyo wake yalisimama ghafla, madaktari wa jumba hili walifika kwenye chumba hicho dakika 2 tu baada ya kuripotiwa. Wakati huo Bw. Leon alikuwa amepoteza ufahamu.
Kusimama ghafla kwa mapigo wa moyo kutaharibu vibaya ogani mbalimbali mwilini, kwa hiyo madaktari walimfanyika Bw. Leon mara moja matibabu ya dharura ya kufufua mapigo wa moyo (cardiac resuscitation), daktari Bi. Chen Xiaohong alisema:
"dakika 12 baada ya kupewa matibabu haya, Bw. Leon alipata fahamu na alianza kupumua na moyo wake ukaanza kupiga."
Baada ya kupewa huduma ya kwanza, Bw. Leon alipelekwa kwenye hospitali maalum ya michezo ya Olimpiki. hatua zote hizo zilichukua dakika 9 tu. Baada ya kufanyiwa upimaji wa dharura na madaktari, Bw. Leon alipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ICU. Baada ya kupewa matibabu kwa siku mbili, hadi kufikia alasiri ya tarehe 21 mwezi huo, Bw. Leon alipona vizuri na kurejea kwenye hali ya kawaida. Bw. Leon alisema:
"madaktari walinipokea vizuri, najisikia vizuri."
Katika muda wa michezo ya Olimpiki ya Beijing, vikundi zaidi ya 30 vya matibabu vilivyoundwa na watu zaidi ya elfu tatu walitoa huduma za matibabu hapo papo kwenye majumba na viwanja vya michezo. Kwa mujibu wa takwimu husika, watumishi hao walitoa huduma kwa watu zaidi ya elfu 20 na kutibu kwa wakati matatizo ya kiafya ya robo tatu ya washirika kwa michezo ya Olimpiki. Aidha, Beijing pia imeweka hospitali 24 maalum kwa ajili ya michezo ya Olimpiki na hospitali hizo zilitoa huduma kwa watu wapatao elfu 5 wanaohusika na michezo hiyo.
Mbali na kutoa matibabu mwafaka na kwa wakati, kazi za huduma za matibabu pia zimeweka rekodi mpya kadhaa kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing. Kwa mfano, matibabu ya jadi ya kichina pia yamechukuliwa na kutumika kwenye huduma za matibabu katika michezo hiyo, ambayo hii ni mara ya kwanza kwenye historia ya zaidi ya miaka mia moja ya michezo ya Olimpiki. imefahamika kuwa watu wanaojitolea zaidi ya 260 wa matibabu ya jadi ya kichina walitoa huduma kwenye majumbe 35 ya michezo na kituo kikuu cha matibabu cha kijiji cha Olimpiki. walitoa huduma za akupancha na usingaji kwa wachezaji, na huduma hizo zilisifiwa sana na wachezaji wa nchi mbalimbali.
Kama ilivyokuwa kwenye michezo ya Olimpiki, katika michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Beijing, watumishi wapatao 2400 wa matibabu mjini Beijing walitoa huduma moja kwa moja kwa wachezaji, waandishi wa habari, watazamaji wa wafanyakazi mbalimbali wa michezo hiyo, vituo 70 vya matibabu ya dharura viliwekwa kwenye majumba ya mashindano na ya mazoezi ya michezo. Kutokana na umaalum wa michezo ya Olimpiki ya walemavu, idara ya huduma za afya ya Beijing pia ilitoa uhakikisho maalum wa matibabu. Huduma maalum za matibabu zilitolewa kwa kulingana na mashindano tofauti na kwa wachezaji wenye ulemavu tofauti.
Katika hospitali ya Xiehe ya Beijing ambayo ilikuwa moja ya hospitali maalum za michezo ya Olimpiki ya walemavu, marekebisho mbalimbali ya kuondoa vikwazo kwa walemavu yalifanyika kwenye vyumba maalum vya wagonjwa. Mwuguzi mkuu Bi. Shen Ning alisema:
"hospitali yetu imeweka vyumba vya wagonjwa visivyo na vikwazo kwa walemavu, chumba cha msalani pia walemavu wanaweza kuingia kwa kutumia viti vya magurudumu, pia ndani kuna viti maalum kwa ajili ya kuoga, wagonjwa wanaweza kuoga wakikaa kwenye viti hivyo."
Ofisa wa idara ya huduma za afya ya Beijing amesema, kazi za uhakikisho wa huduma za matibabu kwenye michezo ya Olimpiki ya walemavu imemalizika vizuri, na juhudi za madaktari ya Beijing zimehakikisha michezo ya Olimpiki ya walamavu ni nzuri kama michezo ya Olimpiki ya Beijing.
|