Familia ya mzee Ma Tingfu wa kabila la Wahui wanaoishi kwenye mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia.
Huu ni mwaka wa kumi tangu familia ya mzee Ma Tingfu wahamie kwenye nyumba mpya. Katika miaka kumi iliyopita, watu wa familia hiyo pamoja na wakazi wengine walibadilisha ardhi yenye hali ya jangwa kuwa mashamba, na wanaishi maisha mazuri. Ingawa wanaishi kwenye kijiji, lakini utajiri wao hata uliwashangaza watu wengi mijini.
Mzee Ma Tingfu mwenye umri wa miaka 74 ana watoto watano wa kiume na wajukuu wa kiume zaidi ya kumi, na baadhi ya wajukuu wake wanafanya kazi ya uchukuzi kwenye sehemu mbalimbali nchini China, mara kwa mara wanawaletea babu na bibi zao matunda na vyakula vingine kutoka nje, pia wanawaelezea mambo ya sehemu za nje. Ingawa iliko kijiji familia ya mzee Ma Tingfu kiko kilomita 127 mbali na Yinchuan, mji mkuu wa mkoa wa Ningxia, lakini maisha ya familia hiyo yanafanana na familia za mijini.
Zamani familia ya mzee Ma Tingfu waliishi milimani, mara kwa mara sehemu hiyo ina hali ya ukame, na waliishi maisha magumu. Miaka kumi iliyopita, familia hiyo ilihamia eneo la uendelezaji wa uchumi liitwalo Hongsibao. Mwanzaoni eneo hilo lilikuwa halina wakazi wengi wala mashamba ya kilimo, lakini hali ya mawasiliano ya barabara ilikuwa nzuri, na jambo muhimu zaidi ni kwamba serikali ilijenga mradi wa umwagiliaji na matumizi ya maji, mzee Ma Tingfu alisema,
"Mwanzoni tulipohamia hapa, hakukuwa na watu wengi, lakini baadaye tulipata maji na umeme. Mbali na hayo barabara na shule zimejengwa, hata msikiti ulikuwa tayari, na mimi nakwenda kufanya ibada mara kwa mara."
Hongsibao ni eneo la wahamiaji kutokana na hali mbaya ya mazingira ya asili lililojengwa na serikali kuu ya China kwa kutenga fedha nyingi. Katika miaka kumi iliyopita, kwa nyakati tofauti, jumala ya wakulima laki mbili walioishi kwenye sehemu zenye ukame wamehamia kwenye eneo la Hongsibao, na kati yao watu wa kabila la Wahui wanachukua asilimia 57. Hivi saa eneo la Hongsibao limegeuka kutoka jangwa kuwa mahali penye miti na chemchem, na kuna nyumba, mashamba na misitu hapa na pale. Mwaka jana inagwa sehemu hiyo ilikumbwa na maafa mabaya ya ukame, lakini wakulima wa eneo la Hongsibao pia walipata mavuno mazuri. Mtoto mdogo wa mzee Ma Tingfu Bw. Ma Yingcheng mwenye umri wa miaka 50 alisema,
"Sisi wakulima wa hapa tunapata ruzuku ya chakula, mbolea ya kemikali, na ruzuku ya maisha kwa watu wa sehemu maskini. Ruzuku hizo kwa jumla ni nyingi sana. Maisha yetu mazuri yanaweza kuhakikishwa."
Licha ya kupanda nafaka, familia ya mzee Ma Tingfu pia wanapanda miti ya matunda. Shughuli za kilimo za aina mbalimbali pamoja na kazi nyingine za uchukuzi na kazi za vibarua mijini zimefanya wastani wa mapato ya wakazi wa eneo la Hongsibao waongezeke kwa mara tano. Bw. Ma Yingcheng ni mmoja kati ya watu waliotajirika katika miaka ya hivi karibuni. Alijenga nyumba kukubwa nzuri, na kuishi pamoja na wazazi wake, ana gari la ujenzi, lori, gari ndogo na pikipiki, na waliwahi kuwapeleka wazazi wao ambao ni waislamu kuhiji Makka mara mbili.
Wakulima wa eneo la Hongsibao pia wamenufaika sana na mfumo wa aina mpya wa matibabu ya ushirikiano vijijini. Mwaka jana mke wa Bw. Ma Tingfu aliugua na tumbo, akatibiwa kwenye hospitali na kugharama yuan 3,800, na alipata ruzuku zaidi ya 3,200 kutoka serikali. Bw. Ma Tingfu alisema,
"Tumejiunga na mfumo wa aina mpya wa matibabu ya ushirikiano vijijini. Watu wenye umri zaidi ya miaka 70 wanatoa yuan kumi kila mwaka, tukipatwa na ugonjwa, tutapewa ruzuku na serikali. Aidha pia tumejiunga na bima kwa watu maskini."
Mwaka jana, jambo la furaha lilitokea kwenye familia ya Bw. Ma Tingfu. Mjukuu wake mdogo zaidi Ma Feng alifanikiwa kuendelea na masomo ya Chuo Kikuu cha Jiolojia cha China.
Ma Feng sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa pili kwenye Chuo Kikuu cha Jiolojia cha China, na yeye ni hodari katika masomo yake tangu alipoanza kusoma shule ya msingi. Katika miaka kumi iliyopita, alijionea mabadiliko ya nyumbani kwake, na kati ya mabadiliko hayo, alijihisi zaidi kwa mabadiliko ya shule. Alisema,
"Nilipohamia kwenye sehemu ya Hongsibao, nilikuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne kwenye shule ya msingi. Wakati huo shule yetu ilikuwa na walimu watatu na wanafunzi zaidi ya 90, na sasa shule hiyo ina walimu zaidi ya 20, na wanafunzi zaidi ya 400."
Ma Feng alisoma kwenye shule ya sekondari ya Liupanshan ambayo ni shule bora zaidi ya sekondari mkoani Ningxia. Kwenye shule hiyo Ma Feng alijionea sera ya upendeleo kwa wanafunzi wa makabila madogo madogo na kutoka sehemu za milimani. Alisema,
"Kwenye shule ya Liupanshan, wanafunzi kutoka vijijini wanapewa ruzuku ya yuan 75 kila mwezi, hawatakiwa kulipa ada ya masomo, wala ya bwenini."
Chuo Kikuu cha Jiolojia cha China Ma Feng anachosoma kiko kwenye mji wa Wuhang ulioko katikati mwa China. Kwa wanafunzi kutoka vijijini, maisha ya mjini ni mazuri zaidi, lakini Ma Feng alisema anakumbuka nyumbani kwake mara kwa mara, kwa kuwa huko kuna familia yake.
2008-10-27
|