Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-19 17:41:02    
Maonesho ya ndege ya Zhuhai yaonesha kiwango cha maendeleo ya teknolojia ya anga ya juu nchini China

cri

Maonesho ya ndege na teknolojia za anga ya juu ya kimataifa ya China yakiwa ni moja ya maonesho matano makubwa ya ndege duniani, hivi karibuni yalifungwa huko Zhuhai, mji ulioko kusini mwa China. kwenye maonesho hayo teknolojia nyingi mpya za ndege na za safari za anga ya juu za China zimeoneshwa, ikiwemo ndege mpya ya kivita ya China J-10. mbali na hayo, ndege ndogo ya abiria iliyotengenezwa na China kwa kujitegemea imeagizwa sana kutoka nchi za nje.

Maonesho ya ndege na safari za anga ya juu ya kimataifa ya China yaani maonesho ya ndege ya Zhuhai ni maonesho maalumu na ya pekee yaliyoidhinishwa na serikali ya China. maonesho hayo yanafanyika kila baada ya miaka miwili kuanzia mwaka 1996, na maonesho ya mwaka huu ni makubwa kabisa kuliko awamu zote zilizopita, makampuni 600 makubwa ya kutengeneza ndege yakiwemo Boing na Airbus yalionesha ndege zaidi ya 60 za kisasa za aina mbalimbali. Ikilinganishwa na maonesho ya awamu zilizopita, watu wengi zaidi walifuatilia na kuvutiwa na bidhaa mpya za China.

Wasikilizaji wapendwa, uliyosikia ni sauti ya ndege mpya ya kivita ya China J-10 ikiruka angani. J-10 ikiwa ni ndege ya kisasa kabisa ya China, ilifanya vitendo mbalimbali vigumu kwa usahihi angani, maonesho hayo yalivutia sana watazamaji.

Bw. Song Wencong ambaye ni msanifu mkuu wa ndege ya J-10 alisema, China ilianza kusanifu ndege ya J-10 miaka ya 80 ya karne iliyopita, na ndege hiyo ni moja ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na juhudi za muda mrefu zilizofanywa na viwanda vya utengenezaji wa ndege vya China kujitahidi kusanifu ndege kwa kujitegemea, ndege ya aina hiyo itainua zaidi uwezo wa kupambana kwa kujilinda wa jeshi la anga la China. Bw. Song Wencong alisema:

"kufanikiwa kwa J-10 kuna umuhimu mkubwa. Inamaanisha kuwa sasa tuna ndege ya kisasa ya kivita. Jambo muhimu ni kwamba unalenga kufikia kiwango cha juu cha kimataifa ulipoanza kazi hii."

Ndege ya J-10 ikiwa ni ndege ya kivita ya kizazi kipya yenye uwezo mwingi, inatengenezwa kwa kutumia usanifu na teknolojia nyingi mpya. katika usanifu wa umbo lake, mabawa na tumbo lake zinaunganishwa kwa pamoja ili kuinua uwezo wa kutogunduliwa kwenye rada na kuongeza ukubwa wa chombo chake cha mafuta. Aidha, ndege hiyo pia ina mfumo wa kisasa wa udhibiti wa urukaji unaofikia kiwango cha kimataifa. Imefahamika kuwa, hivi sasa ndege ya J-10 imeanza kutumiwa kwa wingi na jeshi la anga la China.

Kwenye maonesho hayo, mbali na ndege ya kisasa ya kivita, China pia ilionesha bidhaa mpya na mafanikio mapya yaliyopatikana katika matumizi ya teknolojia za anga ya juu na huduma za safari za anga ya juu. Kati ya majumba matatu ya maonesho hayo, mawili yao yalipewa majina ya "Jumba la ndege za China", na "Jumba la safari za anga ya juu za China". kwenye majumba hayo mawili, makampuni maarufu ya China yalionesha bidhaa zao mpya na za hali ya juu. Msemaji wa kundi la teknolojia za safari za anga ya juu la China Bw. Jia Ke alisema:

"bidhaa zetu zinafunika maeneo ya mfumo wa safari za anga ya juu, mfumo wa silaha za makombora na huduma za safari za anga ya juu, tulionesha matokeo yote mapya tuliyoyapata. Mbali na hayo, pia tulianzisha dhana ya "kikundi cha uokoaji cha anga ya juu", ili kukidhi mahitaji ya maendeleo ya uchumi wa nchi mbalimbali, hasa kazi za kuzuia na kupunguza hasara za maafa na kazi za uokoaji katika hali ya dharura."

Kikundi cha uokoaji cha anga ya juu iliyotajwa na Bw. Jia Ke ni mfumo wa uokoaji wa dharura angani unaosawazisha kwa pamoja raslimali zilizopo za saitelaiti za uongozaji, uchunguzi wa bahari, hali ya hewa na usimamizi wa mazingira ili kuinua kwa ufanisi uwezo wa kukabiliana hali ya dharura ya maafa.

Aidha, katika maonesho hayo ya siku sita, makampuni ya kutengeneza ndege ya China yalisaina makubaliano wa ushirikiano wa teknolojia na ununuzi wa ndege na nchi nyingi. Linalofuatiliwa zaidi ni kwamba kampuni ya ndege za kibiashara ya China itauza ndege 25 ya abiria ya aina ya ARJ21-700 zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 800 kwa kundi la ndege la GE la Marekani. Imefahamika kuwa, hii ni mara ya kwanza kwa ndege za abiria zilizosanifiwa na China kwa kujitegemea kuuzwa kwenye soko la Marekani na Ulaya. Naibu mkurugenzi wa bodi ya kundi la ndege la GE la Marekani anayeshughulikia miradi ya ndege za kiraia Bw. Roger alisema ana imani kuhusu mustakbali wa ndege hiyo kwenye soko. Bw. Roger alisema:

"tunaona kuwa hii ni aina ya ndege iliyopata mafanikio, na itakuwa na mustakabali mzuri wa maendeleo kwenye soko."

Kampuni ya ndege za kibiashara ya China ilidokeza kuwa, baada ya ndege ya ARJ21-700 kumaliza urukaji wake wa kwanza mwezi huu, itaendelea kuruka mara tatu kwa majaribio. Kama hatua hizo zote zikiendelea bila matatizo, tunafikiria kuitoa sokoni."

Msanifu mkuu wa kampuni ya ndege za kibiashara ya China Bw. Wu Guanghui alisema, kwa mujibu wa mpango uliowekwa, China inatumai kuweza kuitoa sokoni ndege kubwa ya abiria iliyosanifiwa kwa kujitegemea na China ifikapo mwaka 2020. Bw. Wu Guanghui alisema:

"tulishirikisha mashirika 49 ya nchini na wataalamu zaidi ya 300 hodari katika kazi za usanifu. Tunataka kuthibitisha mpango wa hatua ya mwanzo ya ndege kubwa ya abiria yenye viti 150 mwishoni mwa mwaka huu."