Waziri mkuu mpya atangazwa DRC
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila amemtangaza waziri mkuu mpya kutoka muungano wa vyama vya upinzani vilivyoshiriki mazungumzo ya kitaifa yaliyomalizika hivi karibuni na kukubaliwa kuundwa kwa Serikali ya mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.
Kwa mujibu wa tangazo kutoka ikulu ya Kinshasa lililosomwa kupitia televisheni ya taifa, Rais Kabila amemteua Samy Badibanga kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.
Badibanga kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni kiongozi wa vyama vya upinzani bungeni.Uteuzi wa Badibanga umekuja baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri mkuu Matata Ponyo, aliyeachia nafasi hiyo Jumatatu ya wiki hii, kufuatia makubaliano ambayo yamepingwa vikali na muungano wa upinzani wa Rassemblement ambao haukushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |