Gambia yatangaza kujiondoa kwa mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC
Gambia imetangaza kwamba itajiondoa kutoka kwa mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC ikiilaumu mahakama hiyo kwa "Mateso na udhalilishaji wa watu wa rangi, hasa Waafrika".
Waziri wa habari Sheriff Bojang amesema kwenye tangazo la runinga ya serikali kwamba mahakama hiyo (ICC) imekuwa ikiwalenga tu viongozi wa Afrika huku ikikosa kuchukua hatua zozote kwa makosa yanayofanywa na nchi au viongozi wa magharibi.
Hatua ya Gambia inakuja baada ya nchi nyingine za Afrika Burundi na Afrika Kusini kutangaza kwamba zinajiondoa kwenye ICC.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |