Kenya yarefusha muda wa kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab kwa miezi sita
Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Bw Joseph Nkaissery amesema Kenya itarefusha muda wa kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab kwa miezi sita, ambayo kwa sasa ina wakimbizi zaidi ya laki 2.6 wa Somalia.
Bw Nkaissery amesema uamuzi huo unatokana na hali mbaya nchini Somalia.
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR pia limeitaka Kenya kuwapatia wakimbizi wa Somalia muda wa kutosha kurudi nyumbani. Serikali ya Kenya imeahidi kushirikiana na Umoja wa Mataifa na serikali ya Somalia, kuweka mpango mwafaka ili kuwarejesha wakimbizi hao kwa amani katika muda huo uliorefushwa.
Mwezi Mei Kenya ilitangaza kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab na kuwarejesha wakimbizi wote wa Somalia kabla ya mwezi Novemba.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |