Watu 50 wafariki kwenye mafuriko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Watu 50 wamefariki Jumanne kwenye mafuriko katika mji wa Boma katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mvua kubwa zimesababisha mto wa Kalamu kuvunja kingo zake na polisi wanasema baadhi yamiili imesombwa na maji hadi nchi jirani ya Angola.
Wakazi wanasema baadhi ya maeneo ya mji huo yamezikwa ndani ya matope.
Gavana wa jimbo la Kongo ya kati Jacques Mbadu amesema kwa kawaida maafa kama haya hutokea kila baada ya miaka 10.
Mara ya mwisho yalitokea mwezi Januari 2015, lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yametokea sasa mwezi ..
Maji ya mto Kalamu yalijaa kimo cha mita mbili (futi sita) juu ya kimo chake cha kawaida.
Mafuriko makubwa, ukame na gharika vinatarajiwa kuongezeaka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |