Vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika vyatwaa mji mmoja kutoka kwa kundi la Al-Shabaab
Jeshi la Somalia na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika AMISOM wiki hii vilitwaa udhibiti wa mji wa Mooragaabey ulioko mkoa wa Bakool, kusini-magharibi mwa Somalia kutoka kwa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab.
Kamanda wa jeshi la Somalia Abdullahi Farah amesema, wapiganaji wa kundi hilo waliondoka katika mji huo wakati vikosi hivyo vilipokuwa vikielekea katika mji huo.
Amesema vikosi hivyo vinafanya operesheni za kuwafurusha na kuwakamata wapiganaji wa Al-Shabaab wanaodhibiti maeneo kadhaa ya mkoa wa Bakool.
Wakati huohuo, jeshi la Somali jana limewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al Shabaab katika operesheni iliyofanyika mjini Mogadishu kufuatia mauaji ya askari mmoja wa jeshi la serikali ya Somalia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |