Askari wa Israel aliyempiga risasi mshambuliaji wa Palestina akutwa na hatia ya mauaji
Mahakama ya kijeshi ya Israel ilitoa uamuzi kuwa askari wa jeshi la nchi hiyo aliyempiga risasi mshambuliaji wa Palestina ana hatia ya kuua bila kukusudia.
Tarehe 24 Machi mwaka jana, wapalestina wawili walimshambulia kwa visu askari mmoja wa Israel huko Hebron, kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wengine.
Kwa mujibu wa hukumu hiyo, mshambuliaji mmoja alilala chini na kupoteza uwezo wa kushambulia baada ya kujeruhiwa vibaya na risasi, lakini wakati huo askari Elor Azaria alimpiga risasi tena kichawani, na hivyo kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.
Kwa mujibu wa sheria za kijeshi za Israel, kosa la kuua bila kukusudia linaweza kuhukumiwa kifungo kisichozidi miaka 20.
Mahakama ya kijeshi nchini humo inatarajiwa kutoa hukumu rasmi kwa Elor Azaria mwezi ujao.
Habari nyingine zinasema, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameeleza kuunga mkono kutolewa msamaha kwa askari Elor Azaria.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |