Mlanguzi El Chapo ahamishwa hadi Marekani
Kiongozi wa genge la walanguzi wa mihadarati nchini Mexico Joaquin "El Chapo" Guzman amehamishwa na kukabidhiwa kwa maafisa wa serikali nchini Marekania mbako atafunguliwa mashataka ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Aliwasili mjini New York kwa ndege kutoka Cuidad Juarez.
Guzman, ambaye huenda akafungwa jela maisha nchini Marekani, amekuwa akisakwa na maafisa wa Marekani kwa tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya.
Anadaiwa kuingiza kiasi kikubwa sana cha dawa za kulevya nchini Marekani.
Kiongozi huyo wa genge la Sinaloa alikuwa anakabiliwa na maombi mawili ya kutaka apelekwe Marekani kujibu mashtaka - moja kutoka California na jingine Texas.
Mwaka uliopita, alihamishiwa gereza la Ciudad Juarez, ambalo linapatikana maeneo ya mpakani karibu na mji wa El Paso katika jimbo la Texas.
Maafisa hata hivyo walikanusha tuhuma kwamba hatua hiyo ilikuwa kama maandilizi ya kumhamishia Marekani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |