Wazima moto 20 wafariki baada ya jengo, kushika moto na kuporomoka Iran
Wazima moto 20 wamefariki baada ya jengo moja kubwa kwenye mji mkuu wa Iran Tehran, kushika moto na kuporomoka.
Wazima moto 200 walikabiliana na moto huo kwenye jengo hilo la ghorofa 17 kwa saa kadha, kabla ya kuporomoka kwa sekunde chache.
Zaidi ya watu 200 pia waliripotiwa kujeruhiwa kwenye mkasa huo.
Jengo hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1962, lilikuwa wakati mmoja jengo refu zaidi mjini Tehran.
Moto huo unaripotiwa kuanza mwendo wa saa 04:30 mapema Alhamisi, wakati watu hawakuwa bado wameingia.
Magari kumi ya kuzima moto yalifika eneo hilo na vituo vya runinga viliripoti kuwa wazima moto kadha walikuwa ndani ya jengo wakati liliporomoka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |