• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 14-Januari20)

    (GMT+08:00) 2017-01-20 18:31:17

    Makamu wa rais wa Burundi atangaza kuondoa askari wa nchi hiyo kutoka Somalia

    Makamu wa kwanza wa rais wa Burundi Gaston Sindimwo ametangaza kuwa nchi hiyo itaondoa askari wake walioko kwenye Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kutokana na Umoja huo kushindwa kuwalipa askari hao.

    Amesema hakuna serikali itakayokubali kuona askari wa nchi nyingine wanalipwa lakini askari wa nchi yake hawalipwi. Amesema kama Umoja wa Afrika umeshindwa kuwalipa, serikali ya Burundi itawaondoa askari hao pamoja na vifaa vyao.

    Tangu mwaka 2007, Burundi imepeleka vikosi sita vyenye jumla ya askari zaidi ya 5,000 nchini Somalia kusaidia kurejesha usalama nchini humo.

    Kwingineko Wapiganaji wanne wa kundi la Al-Shabaab wameuawa na jeshi la Somalia na kikosi cha Umoja wa Afrika AMISOM katika operesheni yao kusini magharibi mwa Somalia. Ofisa mmoja wa majeshi hayo alijeruhiwa kwenye operesheni hiyo. Operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi za vikoso vya usalama za kuimarisha usalama wakati uchaguzi wa bunge unaendelea.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako