Aliyekuwa waziri mkuu wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo amechaguliwa wiki hii kuwa rais mpya wa nchi hiyo.
Aliyekuwa rais Hassan Sheikh Mohamud amekubali kushindwa baada ya kumaliza wa pili kwenye duru ya pili ya uchaguzi.
Farmajo alipata kura 184, Bw Hassan Sheikh akapata kura 97 naye rais mwingine wa zamani Sharif Sheikh Ahmed akapata kura 46.
Mshindi alitakiwa kupata thuluthi mbili ya kura zote zilizopigwa lakini kabla ya duru ya tatu kufanyika, Bw Hassan Sheikh alikubali kushindwa na kumpongeza Farmajo.
Farmajo alihudumu kama waziri mkuu nchini Somalia mwaka 2010 na 2011.
Ushindi wa Mohamed umeendeleza utamaduni wa miaka mingi wa Somalia kutochagua rais aliyepo madarakani.
Sheikh Ahmed alikuwa rais wa Somalia kutoka 2009 hadi Mohamud alipomshinda 2012.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |