Wabunge wa upinzani wa Afrika Kusini wazua vurugu bungeni
Wiki hii kumekuwa na vurugu katika Bunge la Afrika kusini huku wabunge wa upinzani wakipinga hotuba ya Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma.
Wakati akianza kuhutubia alikatizwa na kelele za Wabunge wa upinzani, waliokuwa wakimkosoa.
Miongoni mwa ukosoaji dhidi yake kuhusiana na matatizo ya kiuchumi na rushwa, ulifanywa pia na baadhi ya wabunge kutoka chama tawala.
Awali nje ya bunge la nchi hiyo, Polisi walifyatua mabomu kuwashtua watu waliokuwa wakifanya vurugu, ili kuweza kuwasambaratisha.
Rais Jacob Zuma alipeleka kikosi cha wanajeshi zaidi ya elfu nne bungeni hapo ili kulinda usalama, wakati akitoa hutuba yake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |