Mohamed Abdullahi Mohamed aapishwa kuwa rais mpya wa Somalia
Bw. Mohamed Abdullahi Mohamed anayejulikana kwa jina la Farmajo ameapishwa wiki hii kuwa rais mpya wa Somalia katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa kanda hiyo walioahidi kuunga mkono serikali mpya ya nchi hiyo.
Viongozi kutoka Djibouti, Kenya, Sudan, Uganda na Ethiopia wamehudhuria hafla hiyo iliyofanywa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu.
Baada ya kuapishwa kuwa rais wa tisa wa Somalia, rais Farmajo ameahidi kurejesha heshima ya nchi hiyo kwa kutatua changamoto za kiusalama na kiuchumi zinazoikabili nchi hiyo.
Bw Farmajo aliyechaguliwa kuwa rais Februari 8, ameapa kuweka kipaumbele katika usalama, huku akisema serikali yake itafanya juhudi kukabiliana na msukosuko uliosababishwa na ukame, kujenga imani na kutatua changamoto za kiuchumi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |