Wahamiaji 13 wakutwa wamekufa ndani ya kontena nchini Libya
Miili ya wahamiaji kumi na tatu waliokufa baada ya kukosa hewa imekutwa ndani ya kontena magharibi mwa Libya hayo ni kwa mujibu wa shirika la Msalaba Mwekundi limesema Alhamisi wiki hii.
Kwa mujibu wa shirika hilo, waathirika walionekana kuwa walifungiwa ndani ya kontena kwa siku kadhaa wakati kontena hiyo ilikuwa ikipelekwa katika mji wa pwani wa Khoms ambapo walikua walipanga kushuka ili kuelekea Ulaya.
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema katika taarifa yake kwamba wahamiaji wengine Hamsini na sita waliokolewa, huku baadhi yao wakiwa na majeraha makubwa,
Libya imekuwa ni sehemu ya watu wanaopitia kwa kutafuta kufika Ulaya katika mazingira hatari ya maisha yao. Kwa mujibu wa serikali ya Itali, wahamiaji 181,000 kati yao walifika mwaka jana katika pwani ya Italia baada ya kuvuka bahari ya Mediterranean.
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linasema kwa upande wake kwamba zaidi ya wahamiaji 4,500 walifariki mwaka 2016 wakijaribu kuvuka bahari hiyo.
Wiki hii, miili ya wahamiaji 74 iligundua katika pwani ya magharibi ya Tripoli. Kwa mujibu wa kikosi cha ulinzi katika pwani ya Libya , wapita njia waliiba injini ya boti yao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |