Umoja wa Mataifa warefusha kwa mwaka mmoja muda wa vikwazo dhidi ya Yemen
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kurefusha kwa mwaka mmoja hadi tarehe 26 Februari mwakani, vikwazo dhidi ya Yemen, kutokana na hali ya nchi hiyo kuendelea kuwa tishio kwa amani na usalama duniani.
Baraza hilo limekubali kuchukua hatua za kuzuia mali na kuweka marukufu ya kusafiri dhidi ya watu binafsi ua mashirika yanayoharibu mchakato wa amani nchini Yemen. Pia linafuatilia changamoto za kisiasa, kiusalama, kiuchumi na za kibinadamu zinazoikabili Yemen, pamoja na matishio yanayotokana na usafirishaji haramu, ukusanyaji na matumizi mabaya ya silaha.
Baraza hilo limesisitiza tena ahadi yake ya kutimiza umoja, mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi ya Yemen, na limetoa wito kwa pande zote za Yemen zitatue mgogoro kwa njia ya mazungumzo, na sio matumizi ya nguvu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |