Kenya na Somalia zaahidi kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi
Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed amefanya ziara rasmi ya siku tatu nchini Kenya ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu achaguliwe kuwa rais.
Alitunukiwa heshima ya kijeshi ya mizinga 21.
Baadaye yeye na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta walifanya mazungumzo kuhusu jinsi ya kuboresha uhusiano kati ya Nairobi na Mogadishu.
Kenyatta amewaambia waandishi wa habari wamekubaliana kuanzishwa kwa Safari za ndege za moja kwa moja kati ya Nairobi na Mogadishu.
Aidha waliahidi kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi, kwa kupambana bila huruma na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab, ambao wameongeza mashambulizi ya kigaidi kwenye nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Rais Mohamed ameipongeza Kenya kwa mchango wake mkubwa kwenye mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |