Rwanda yatahadharisha kuhusu itikadi ya mauaji ya kimbari siku chache kabla ya kumbukumbu ya mauaji hayo
Kumbukumbu ya miaka 23 tangu yatokee mauaji ya halaiki nchini Rwanda itafanyika Aprili 7, huku mkazo ukiwekwa kwenye kupambana na itikadi ya mauaji hayo.
Kamati ya taifa ya kupambana na mauaji ya kimbari ya Rwanda, imesema kumbukumbu hiyo itafanyika kwa kauli mbiu ya "kumbuka mauaji ya halaiki dhidi ya watutsi, pambana na itikadi hiyo, na imarisha maendeleo".
Akiongea kabla ya maadhimisho ya siku hiyo Katibu mkuu wa kamati ya kupambana na mauaji ya halaiki Dk. Jean Damascene Bizimana, amesisitiza dhamira ya serikali kupambana na itikadi hiyo. Amesema utawala bora, maendeleo endelevu na kuwakumbuka waliopoteza maisha yao kwenye mauaji hayo, ndio silaha ya Rwanda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |