• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Machi-24 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-24 18:08:57

    Watu 10 wauawa kwenye shambulizi la Al Shabaab kusini mwa Somalia

    Watu 10 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab kusini mwa Somalia.

    Mkuu wa Wilaya ya Barawe Bw Aden Omar Madobe amesema wapiganaji watatu, wanajeshi wanne wa serikali na raia watatu ndio waliouawa kwenye shambulizi hilo. Bw Madobe amesema kundi la Al Shabaab halijaweza kutwaa udhibiti wa wilaya hiyo, lakini amesema lilijipanga vizuri kwenye shambulizi lao.

    Shambulizi hilo limetokea wakati Somalia inaendelea kukumbwa na msukosuko mkubwa wa kiafya na njaa inayoweza kutokea wakati wowote. Changamoto nyingine kubwa ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu unaoathiri mikoa 11 kati ya 18.

    Kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa mataifa Bw Liu Jieyi amesema Somalia imeingia katika kipindi muhimu cha kujenga taifa, lakini inahitaji msaada kukabiliana na changamoto mbalimbali.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako