• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Machi-31 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-31 20:06:38

    Mke wa aliyekuwa rais wa Cote D'Ivoire aachiliwa huru

    Mahakama kuu jijini Abidjan nchini Cote D'Ivoire imemuachilia huru Simone Gbagbo mke wa Laurent Gbagbo rais wa zamani wa nchi hiyo anayeshikiliwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC.

    Kesi ya Simone imekuwa ikiendelea kwa zaidi ya miezi 10 na Majaji wameamua kuwa hakuna ushahidi kuonesha kuwa alichochea kuuawa kwa rais nchini humo.

    Muungano wa mashirika ya waathirika wa vurugu na machafuko ya nchini humo wamesema wamehuzunishwa na hatua hiyo na kutaka Simone afikishwe katika Mahakama ya ICC kushtakiwa na mumewe.

    Mwanasheria mkuu wa serikali Ali Yee amesema, huenda uamuzi huu wa Mahakama ukawa ni ujumbe kwa wanasiasa kuelekea katika maridhiano.

    Simone wakati wote alikuwa anakusha madai ya kuhusika katika machafuko na kesi hiyo ilikuwa ni ya kisiasa.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako