Bunge la Somalia laidhinisha orodha ya baraza jipya la mawaziri
Bunge la Somalia limeidhinisha orodha ya baraza jipya la mawazari iliyotangazwa na waziri mkuu wa Somalia Bw Hassan Ali Kheyre wiki iliyopita.
Katika kikao cha bunge kilichofanyika jana, wabunge 241 walipiga kura 224 za ndio, kura 15 za hapana, na wengine wawili hawakupiga kura.
Bw Kheyre amesema serikali ya Somalia itachukua hatua haraka iwezekanavyo, ili kutatua changamoto zinazoikabili Somalia. Mkutano wa kwanza wa baraza la mawaziri utafanyika wiki hii, ukifuatilia zaidi masuala ya usalama na ukame.
Bw Kheyre alitangaza orodha ya baraza jipya la mawaziri tarehe 21 mwezi huu, likiwa na mawaziri 41 na manaibu 26. Bw Gouled Hassan Dourad ameteuliwa kuwa naibu waziri mkuu wa Somalia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |