Mkutano wa kilele wa Umoja wa nchi za kiarabu wasisitiza kuunga mkono pendekezo la amani la nchi za kiarabu
Mkutano wa 28 wa kilele wa nchi za kiarabu umekamilika wiki hii nchini Jordan, na kutoa taarifa ya Amman, inayosisitiza kuwa suala la Palestina bado ni ajenda kuu ya dunia ya kiarabu.
Mkutano huo umesema utaendelea kuunga mkono pendekezo la amani la nchi za kiarabu lililotolewa mwaka 2002, na kutoa mwito wa kuhimiza utekelezaji wa azimio namba 2334 la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Taarifa pia imesema nchi za kiarabu zitaendelea kufanya juhudi ili kuzindua mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel kwenye msingi wa Ufumbuzi wa kuwepo kwa nchi mbili.
Kwenye mkutano huo Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, Ufumbuzi wa nchi mbili ni njia pekee ya kutatua mgogoro kati ya Palestina na Israel. Ameitaka jumuiya ya kimataifa ifuatilie hali inayowakabili wapalestina, na kutaka kusitishwa kwa hatua za upande mmoja zitakazoharibu ufumbuzi huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |