Marais wa China na Marekani waandaa mazungumzo
Rais Xi Jinping wa China amezuru Marekani, kwa mkutano wa kwanza na mwenzake wa Marekani Bw. Donald Trump, unaolenga kuelekeza uhusiano wa nchi mbili.
Katika ziara hiyo ya siku mbili, Rais Xi amekutana na Bw. Donald Trump, ambapo watabadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani na masuala ya kikanda na ya kimataifa. Rais Xi pia anatarajiwa kuhudhuria tafrija ya kumkaribisha iliyoandaliwa na rais Trump wa Marekani.
Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko katika ziara ya siku mbili nchini Marekani, amekutana na rais Donald Trump na viongozi hao kufanya mazungumzo ya kina na ya kirafiki.
Katika mazungumzo yao, marais hao wamesifu maendeleo ya uhusiano kati ya nchi zao na wamekubaliana kuusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo upate mafanikio makubwa zaidi na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili na watu wa nchi zote duniani.
Rais Xi amesema ushirikiano ni chaguo pekee sahihi la China na Marekani, nchi ambazo zinaweza kuwa wenzi wazuri wa ushirikiano, na kwamba pande hizo mbili zinapaswa kupanga mawasiliano kati ya viongozi wa nchi hizo. Rais Xi amemkaribisha rais Trump kufanya ziara rasmi nchini China ndani ya mwaka huu.
Rais Trump amesema Marekani na China zinabeba majukumu makubwa kwa kuwa nchi kubwa kiuchumi duniani, hivyo pande hizo mbili zinapaswa kufanya mawasiliano na uratibu katika masuala muhimu ili kupata mafanikio makubwa zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |