Umoja wa Mataifa wafuatilia shambulizi la silaha za kemikali lililotokea nchini Syria
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres ametoa taarifa kupitia kwa msemaji wake, akionyesha wasiwasi kuhusu matumizi ya silaha za kemikali kwenye shambulizi la anga lililotokea mkoani Idleb nchini Syria, na alitoa salamu za pole kwa wahanga na jamaa zao.
Taarifa imesema kwa sasa Umoja wa Mataifa hauwezi kuthibitisha peke yake undani wa shambulizi hilo. Kikundi cha uchunguzi cha silaha za kemikali cha Umoja wa Mataifa kimeanza uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Makao makuu ya shirika la ufuatiliaji wa haki ya binadamu la Syria yamesema, ndege za kivita zilitumia gesi yenye sumu katika shambulizi hilo na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 58, na wengine wengi kujeruhiwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |