Watu 11 wauawa katika shambulizi la mabomu St.Petersburg, Russia
Shambulizi la mabomu lililotokea jana mchana katika subway mjini St.Petersburg nchini Russia limesababisha vifo vya watu 11 na wengine 45 kujeruhiwa.
Msemaji wa Idara kuu ya kuendesha mashtaka ya Russia amelitaja tukio hilo kuwa ni shambulizi la kigaidi, na kusema uchunguzi umeanza ili kuhakikisha shambulizi lolote la kigaidi kama hilo halitokei tena.
Shambulizi hilo limetokea jana mchana ndani ya behewa moja la subway iliyokuwa njiani kati ya vituo vya Sennaya Ploschad na Chuo cha Teknolojia. Njia hiyo ya subway ambayo ilifungwa kwa muda imeanza tena kazi.
Rais Vladimir Putin wa Russia ameweka shada la maua katika eneo kulikotokea mlipuko kwenye subway na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulizi hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |