Zaidi ya wafungwa 4,600 watoroka jela ya Makala nchini DRC
Zaidi ya wafungwa 4,600 wametoroka wiki hii kutoka jela ya Makala nchini DRC
Wakazi wengi mjini Kinshasa walilazimika kurudi nyumbani mapema siku ya Jumatano, baada ya kutoroka kwa wafungwa hao.
Wakazi wa mji wa Kinshasa walichukua tahadhari hiyo ili kuepuka kufananishwa na wahalifu ambao walitoweka baada ya mashambulizi dhidi ya jela kuu ya Makala, ambao polisi imeendelea kuwasaka. Jela hiyo ina uwezo wa kupokea wafungwa 1,500, lakini inaarifiwa kuwa ililikua na wafungwa zaidi ya 7,000.
Kwa mujibu wa polisi, wafungwa wengi hatari na wahusika wa uhalifu mkubwa pia walitoroka.
Wito tayari umetolewa ili kuwafichua wahalifu hao ambao huenda wamejificha katika vitongoji vya mji wa Kinshasa.
Jela ya KRPF, inayojulikana kama jela kuu ya Makala ilijengwa katika enzi za ukoloni, na imekua na tatizo kwa muda mrefu la kupokea wafungwa wengi.
Maafisa kadhaa na mashrika yasiyokua ya kiserikali yalielezea matatizo yanayoikabili serikali kwa kuhudumia maelfu ya wafungwa katika jela hiyo, ambapo wengi wao walikua wakizuiliwa kwa muda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |